Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Na mkutano huo unaoongozwa na mkuu wa ukoo kwa upande wa kiumeni, naye huuliza kama kilio au maombolezo yameisha.! Kama watasema yaendelee, basi anaruhusiwa kuuendeleza kwa gharama zake, na kama utakuwa umefika mwisho, basi mjadala wa urithi unafanyika kwa kutoa mapendekezo na maafikiano yaliyopatikana katika kikao cha uficho.
 
Endapo akina mama wamekubaliana na uteuzi wa mrithi, basi mama mmoja huchaguliwa kufagia eneo ambalo mfiwa alikuwa analala, ambapo kama mrithi ametoka upande wa kiumeni basi mfagiaji huwa wa upande wa kikeni na lazima pafagiliwe siku hiyo hiyo.
 
Baadaye watu wote hutangaziwa mrithi ni nani na hapo hutolewa chakula na baada ya chakula watu huondoka.
Kayeemba hupewa nafasi ya kumnawisha mrithi miguu, mikono na uso kwa maji ya uvuguvugu na kisha humpaka mafuta; ikiwemo Vifaa vyote ambavyo vimerithishwa navyo pia hupakwa mafuta.
 
Tendo hilo likishafanyika, hutolewa nje viti viwili vinavyokaliwa na mrithi na mrithiwa na hii inakuwa fursa ya kupewa mawaidha kwa lugha ya Wafipa huita ‘Ukusuunda’ na baada ya mawaidha hayo kutolewa hufuatiwa na kitendo cha kunyolewa nywele wahusika.
 
Kwa Wafipa kuonesha huzuni ya kufiwa, wote hupaswa kunyoa nywele zote kichwani (kipara) na hili hufanyika kwa ndugu wote wa marehemu, ambapo Kwa kawaida mrithi na mrithiwa hupaswa kunyoana wenyewe, kisha baada ya kumaliza msiba ilikuwa ni shurti kuenda kuoga maji ya mtoni
 
Baada ya hapo kinatolewa chakula cha jioni. ‘i chiloosha’. Mkuu wa ukoo wa upande wa baba alikula kuku na kwa heshima sana alipewa filigisi ‘i’inkushu’ ambayo kwa Wafipa ni
nyama ya heshima sana (hailiwi na wote). Naye humega na kugawa kidogo kidogo kwa baadhi ya wanaukoo.
 
Mjumbe au mkuu wa kijiji naye alichinjiwa kuku, ikiwa ina maana kuku wa kusafisha mji, na huyo kuku aliliwa na jumbe pamoja na wazee wengine wa kijiji ili kukisafisha hicho kijiji. Hii kwa wale wapenda kuku, siku kama hizo hawazikosi….

Moto wa kilioni pia huzimishwa siku hiyo na mzimishaji huwa ni kayeemba, na Majivu yote hutupwa chooni pia. Kuzimwa kwa moto huo huonesha kwamba kilio kimeisha.
 
.
Screenshot_20190621-024916_Facebook.jpeg
 

Attachments

  • FB_IMG_1561074647653.jpeg
    FB_IMG_1561074647653.jpeg
    52.5 KB · Views: 21
Back
Top Bottom