Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

UHUSIANO AFYA YA KINYWA NA MENO
Afya ya meno na kinywa kwa ujumla inahusiana na afya ya mwili mzima kwa njia tofauti, na aina ya vyakula unavyopendelea kula; sababu kuwa na uwezo wa kutafuna chakula na kukimeza ni muhimu ili mwili wako uweze kupata virutubisho muhimu vya kujenga mwili.
 
Halikadhalika kuwa na kinywa chenye matatizo huweza kuathiri namna mtu anavyozungumza na hata kujiamini kwake mbele za watu walio karibu, kupunguza ufanisi kwa wanandoa, pia matatizo hayo ya meno yanaweza kupelekea gharama kubwa ya matibabu na ukarabati wa meno yako.

SABABU ZINAZOPELEKEA KUATHIRI AFYA YA KINYWA NA KUTOA HARUFU MBAYA MDOMONI
 
Baadhi ya watu ambao hupendelea kula mara kwa mara vyakula venye sukari nyingi na vyenye siagi, imeeleza na wataalamu kuwa watu hao kwa asilimia kubwa ndio wamekuwa wakisumbuliwa zaidi na matatizo haya, kwani huzalisha kemikali nyingi mdomoni ambazo huruhusu wingi wa asidi au tindikali ambayo nayo humpelekea muhusika kujawa na mate mengi mdomoni.
 
Ambapo kujawa mate huko mdomoni hupelekea kukosa kujiamini kwa muhusika mbele ya wenzao, iwe wakati wa kuongea au kucheka kwani wamekuwa wakirusha chembe-chembe za mate ambazo huwatoka vinywani mwao pasipo wao wenyewe kujitambua au kuweza kujizuia, na ikifikia wakati huo watu hawa ndio hutengwa waziwazi na wenzao.
 
Ambapo kutokana na nyufa zilizoko katikati ya meno huruhusu mabaki mengi ya vyakula kutwama kwa muda mrefu, na kutoa ulinzi kwa baikteria shambulizi wa meno kutoshambuliwa na tindikali-mate, kwani wakati muhusika akiswaki au kusafisha kinywa chake hushindwa kuzisafisha sehemu hizo zenye mabaki ya vyakula.
 
KUNUKA KWA MDOMO NA NAMNA SAHIHI YA KUZUIA HARUFU MBAYA YA KINYWA

Kutoa harufu mbaya kinywani, huchagizwa na kutokupiga mswaki mara kwa mara, kutumia mswaki mmoja muda mrefu, kutojiwekea utaratibu wa kusafisha mabaki ya chakula yaliyotwama katikati ya meno yako au kwenye fizi.
 
Back
Top Bottom