Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Maskini na Tajiri
Maskini na tajiri wana mawazo tofauti. Maskini hudhani utajiri ni chanzo cha matatizo. Tajiri hudhani umaskini ni chanzo cha matatizo. Maskini hudhani ubinafsi ni kitu kibaya. Tajiri hudhani ubinafsi ni kitu kizuri.

Maskini ana mawazo ya kupata pesa bila kufanya kazi. Tajiri ana mawazo ya kupata pesa kwa kufanya kazi. Maskini hudhani tajiri ana tabia ya kuringa. Tajiri hupenda kuzungukwa na watu sahihi wenye mawazo sawa na ya kwake.
 
Maskini hutengeneza pesa kwa kufanya kazi asizozipenda. Tajiri hutengeneza pesa kwa kufanya kazi anazozipenda. Maskini hudhani kuwa tajiri lazima usome sana. Tajiri hudhani kuwa tajiri si lazima usome sana.

Maskini hutamani mambo mazuri ya wakati uliyopita. Tajiri hutamani mambo mazuri ya wakati unaokuja. Maskini huamini ili uwe tajiri lazima ufanye kitu fulani. Tajiri huamini ili uwe tajiri lazima uwe kitu fulani.
 
 
1. Huongeza furaha ya moyo(piece of mind)
Kusamehe mtu mwingine humfanya mtu huyo kuwa huru kwa kila jambo ambalo analifanya. Kwani kama nilivyosema hapo awali ya kwamba watu wengi tumebeba mizigo mizito ndani ya nafsi zetu, hata hivyo kutoka na mizigo hiyo mizito tunashindwa kupiga hatua za kimafanikio. Hivyo ili kuweza kupiga hatua za kimafanikio hatuna budi kuweza kujifunza kuweza kuwaaemehe watu wengine waliowahi kutokosea . Hata vitabu vya dini vinatukumbusha ya kwamba Mungu tabia yake kusamehe hivyo nasi hatuna budi kusamehe wengine. Vitabu hivyo hivyo vya dini vinasema ya kwamba saba Mara sabini. Na endapo utasamehe unafungua milango ya mafanikio yako.
 
Maskini hupenda kuburudishwa kuliko kuelimishwa. Tajiri hupenda kuelimishwa kuliko kuburudishwa. Maskini ana woga. Tajiri hana woga.

Maskini hufundisha watoto wake jinsi ya kupambana na maisha. Tajiri hufundisha watoto wake jinsi ya kuwa matajiri. Maskini hana nidhamu ya mapato na matumizi. Tajiri ana nidhamu ya mapato na matumizi.

Maskini hufanya kazi kwa bidii kupata pesa. Tajiri hutumia pesa kupata pesa. Maskini ni mdogo kuliko matatizo yake. Tajiri ni mkubwa kuliko matatizo yake.
 
2. Kusamehe ni njia ya mafanikio.
Endapo leo utaamua kusamehe ni ishara ya kwamba utaonfokana katika sakata la kuwa katika wimbi la mawazo , hata hivyo kupelekea wewe kuwa na mawazo chanya, mara kadhaa watu ambao hawana ule moyo wa msamaha kwa namna moja ama nyingine huwa hawapo sawa kwani huwa hawa amani hata kidogo, hata hivyo kama kweli uyataka Maisha yawe sawa ni muda wako sahihi wa kuvutua vile vyote vilivyomo katika nafsi yako kinyume cha hapo utakuwa unapotea hajalishi ulikwazika kwa kiasi gani. Pia ukumbuke wabaya watu, pia watu hao hao ndio wazuri na wana mchango mkubwa katika safari yako ya mafanikio.
 
Maskini huamini unahitaji pesa kupata pesa. Tajiri huamini utapata pesa kwa kutumia pesa za wengine. Maskini ana wivu wa chuki. Tajiri ana wivu wa maendeleo.

Fikiri kama anavyofikiri tajiri. Ukifikiri tofauti na anavyofikiri tajiri, utakufa maskini.

Maskini: umaskini ni chanzo cha matatizo, ubinafsi ni kitu kizuri, kuwa na mawazo ya kupata pesa kwa kufanya kazi, penda kuzungukwa na watu wenye mawazo sawa na ya tajiri.

Tengeneza pesa kwa kufanya kazi unazozipenda, kuwa tajiri si lazima usome sana, tamani mambo mazuri ya wakati unaokuja, kuwa tajiri lazima uwe kitu fulani.
 
3. Kusamehe huimarisha afya.
Afya njema ni njia ya kupata Mafanikio, moja ya kanuni ya kutaka kupata Mafanikio ni kwamba unahitaji kuwa na afya njema ili uweze kuimarika na kupata Mafanikio hayo. Hebu tutafakari kidogo hivi leo ukipata ugonjwa wowote na kukufanya usiweze kuendelea na kazi yako hivi huwa unaathirika kwa kiasi gani katika jambo lako? Kama umepata majibu Nafikiri utakuwa umeona umuhimu wa kuwa na afya njema.
 
Penda zaidi kuelimishwa kuliko kuburudishwa, usiwe na woga, fundisha watoto wako jinsi ya kuwa matajiri, kuwa na nidhamu ya mapato na matumizi.

Tumia pesa kupata pesa, kuwa juu ya matatizo yako, amini utapata pesa kwa kutumia pesa za wengine, kuwa na wivu wa maendeleo.

Hivyo, chukia umaskini, jiangalie wewe kwanza na familia yako, fanya kazi kwa bidii na maarifa, usiwe mzururaji, tumia vipaji ulivyopewa na Mungu.

Hutafikia malengo yako kikamilifu bila msaada wa wataalamu, zifanyie kazi ndoto zako za baadaye.
 
Watu wengi hawana hamasa za kiutendaji wa mambo mbalimbali kwani dhahiri ya kwamba miili yao tayari imeathiriwa na magonjwa mbalimbali yatokanayo na mawazo ambayo yamesabishwa na watu wanaokuzunguka. Kuna magonjwa ambayo Mara nyingi husababishwa na mawazo kama vile pressure.
 
Hivyo enadapo utamua kuwasamehe watu wengine ambao waliwahi kukosea unaweza kuwa katika misingi ya kuimarika kiafya kiujumla, na kufanya hivyo kutakufanya uweze kuongeza uwezo wako wa kufikiri hata kukupelekea kuweza kupiga hatua za kimafanikio.

Hivyo tambua na elewa inahitajika nguvu ya msamaha ambayo leo itakufanya uweze kupata Mafanikio ya kweli.
 
Tangaza biashara yako, jinyime kwa mengi, usiogope kufanya jambo lolote lenye tija ulilolipigia hesabu, wape watoto wako kila kitu isipokuwa umaskini, mali bila daftari hupotea bila habari.

Fanya biashara, geuza matatizo yako kuwa changamoto, kopa pesa kupata pesa, kuwa na upendo kwa maskini wenzako na kwa matajiri wenzako watarajiwa.

Tajiri: bila maskini wewe ni maskini na bila tajiri maskini ni tajiri. Tajiri akiwa na maadili, maskini atakuwa tajiri.
 
Back
Top Bottom