Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

heheheheeeeeeee hii serikali inafurahisha kweli.
hivi walimchangia angalau pesa ya kununulia boxer?
walimchangia hela ya kununua gloves?
walimchangia hela ya nauli?
walimchagia hela ya kifungua kinywa?
walimchangia hela ya kondomu itakayomsaidia kuitambulisha nchi kwenye pambano pendwa?

kama safari yake ilikuwa na baraka za serikali kimsaada basi sawa wana haki ya kumuangushia shutuma bwana bondia.
sioni ajabu bondia kupigwa round ya pili huwezi jua mara jamaa alishikwa na tumbo la kuharisha hivyo basi akaona ni bora apokee aibu ya kupigwa mapema kuliko kubeba aibu ya kumwaga kinyesi cha pilau la mbuzi hadharani.

Waziri wa michezo wa Tanzania Harrison Mwakyembe ametaka shirikisho la mchezo wa ndondi nchini humo kumuadhibu mwanamasumbwi Selemani Bangaiza kwa kukatiza mapigano katika raundi ya pili bila kuonyesha juhudi zozote, ameieleza BBC mkuu wa shirikisho hilo.
Mwakyembe amemshutumu bondia huyo kwa kutojitahidi kwa kutosha na kutoiwakilisha Tanzania vema.
 
Mamilioni ya watu wamechepuka katika mahusiano yao. Wengine wameua na imebaki kuwa siri yao. Wengi wanakwepa kodi ya serikali na hawakamatwi. Lakini hatuwezi kumdanganya Mungu. Kwa sababu anatujua hadi ndani ya mioyo yetu.

Mioyo yetu wenyewe hutudanganya kidogokidogo katika kutenda dhambi, wakati mwingine bila sisi wenyewe kujua. Lakini, iamini Biblia, Mungu hawezi kuichukulia dhambi kirahisirahisi! Kwa sababu anaupenda sana uumbaji wake.
 
Kuna kitu kibaya sana ndani ya mtu. Hilo liko wazi. Biblia inasema chanzo cha matatizo ya mtu ni moyo wake, roho yake, pamoja na uwezo wake wa kufikiri. Tumejaa ulaghai, unafiki na utata. Tunajichezea sisi wenyewe ule mchezo wa kitoto wa kombolela. Yaani, tunajificha na kujitafuta wenyewe, tunawadanganya watu lakini Mungu anatuona.

Labda ni katika mazingira hayo ambapo moyo hufanya kazi yake kwa uharibifu zaidi. Huficha uovu mkubwa wa dhambi unaoendelea kuwa mkubwa, na matokeo yake kuwa mabaya na mazito zaidi. Moyo unatulaghai katika kufikiri kuwa si mbaya, au kwamba Mungu ni mwenye huruma sana kiasi kwamba atapuuza.
 
Tusipoacha kutenda dhambi, dhambi haitakomeshwa. Ni wajibu wa kila mmoja wetu kukomesha dhambi katika maisha yake. Usisubiri wengine waikomeshe kabla au kwa niaba yako. Hata serikali haitaweza kukusaidia.

Kuna namna moja tu ya kukomesha dhambi, nayo ni kufunga milango yote ya dhambi baada ya kumkaribisha Mungu katika maisha yako.

Funga milango yako yote ya dhambi na kaa mbali na nyavu zinazowinda watu kabla miguu yako haijanaswa na nyavu hizo.
 
Mungu ni mkamilifu milele. Anaishi katika ukamilifu wa milele. Hivyo, kabla ya uumbaji, aliishi katika ukamilifu, baada ya uumbaji, ataishi katika ukamilifu.

Ukiichunguza sana hii kauli utajua Mungu ni nani. Mungu ni Muumbaji, aliyekuwepo, aliyepo, na atakayekuwepo.

Hapa duniani kuna watu wawili tu: Mungu na wewe! Wengine wote, vingine vyote, wako au viko kisogoni mwako. Nje ya macho yako kuna Nuru. Nuru hiyo ndiye Mungu. Wengine wote, vingine vyote, ni akisi ya taswira ambazo ziko ndani yako; ambazo unatakiwa kuziona nje ili uone umekosea sehemu gani, na uweze kurekebisha dunia yako ya ndani.
 
Wale wanasiasa wanaotwambia kila siku kuwa tulete mabadiliko duniani wanajisumbua iwapo hawatatwambia tulete mabadiliko ndani ya dunia zetu za ndani kwanza. Ukibadilisha dunia yako ya ndani, utabadilisha dunia yako ya nje.

Kwa nini? Kama Mungu yupo, yuko wapi? Kwa nini asijionyeshe ili nasi tumwone? Kama alituumba, kwa nini hatuonani naye uso kwa uso? Kwani tatizo ni nini? Faida ya yeye kutojionyesha kwetu ni nini?

Mungu hawezi kujionyesha kwetu kwa kuwa asili yetu ya ubinafsi itasababisha mtafaruku na matatizo makubwa dunia nzima. Kila mtu duniani kote atamng’ang’ania, atamtamani sana, na hakuna la maana litakalofanyika. Itakuwa kinyume na kusudi la maisha; na kusudi la maisha ni kuishi naye mbinguni kwa furaha ya milele, na hatutaweza kuishi naye mbinguni iwapo tuliishi naye duniani.
 
Kiburi ni kiwango cha juu kabisa cha umimi au ubinafsi, na ni sumu ya mahusiano.

Kuwa na kiasi. Usiwe mjinga sana wala usiwe mjanja sana. Ukiwa mjinga sana utapata matatizo, kwa Mungu na kwa wanadamu, na ukiwa mjanja sana utapata matatizo pia, ambayo ni kiburi, kwa sababu mtu mwenye kiburi hawezi kamwe kuridhika na heshima na unyenyekevu anaoupata kutoka kwa watu.
 
Watu wenye kiburi ni wabinafsi, watu wanaopenda kuheshimiwa na kunyenyekewa, na wanajiona bora zaidi kuliko wengine, wanaopata taabu sana kuomba msamaha. Kiburi si upendo na upendo si kiburi. Dawa ya kiburi si kiburi kingine. Dawa ya kiburi ni upendo na hekima.

Hata hivyo, kuna tofauti kati ya kutokujiamini na kiburi. Mtu anaweza asijiamini na asiwe na kiburi, na anaweza asijiamini na akawa na kiburi.

Wengine wanasema kiburi ni kizuri, kwamba ili umshinde Shetani lazima uwe na kiburi. Lakini kiburi dhidi ya Shetani unakishinda kwa hekima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…