Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Muache aende zake kwani huenda kuendelea kuwa naye ndiyo kuyafupisha maisha yako. Inawezekana kuna mambo mazuri ambayo amekuwa akikufanyia huko nyuma kiasi kwamba ukikumbuka unasita kufanya maamuzi ya kumtosa.
 
Sikiliza nikuambie kitu, unapokutana na hali hiyo elewa ni shetani ambaye anataka kukufanya uendelee kuwa kwenye utumwa wa mapenzi. Pata ujasiri, yaliyopita katika uhusiano wako, yafanye kuwa historia kisha fanya uamuzi sahihi.
 
According to her, she is now a statistic for being ‘one of those strong independent women who is unmarried at 40’. The writer added that the realisation brings her joy.
 
Uamuzi sahihi ni upi? Sidhani kama hapa panahitaji darasa zito. Uamuzi wa kwanza ni kukubali kuendelea kuwa kwenye uhusiano huo. Utaamua hivyo kama utaona kwamba uko tayari mapenzi yakuue lakini siyo kumuacha huyo uliyetokea kumpenda.
 
Ila kumbuka wanaochukua uamuzi huu ni malimbukeni wasiyoyathamini maisha yao. Uamuzi mwingine ambao naona ni sahihi ni ule wa kumuacha aende kisha wewe uyaache maisha yako yaendelee kuwepo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…