Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Lakini, sasa kutokana na bei anayouzwa Zaha na klabu yake ya Crystal Palace jambo hilo linawafanya Arsenal kuwa na chaguo moja tu la kumpiga mshambuliaji wao, Mwaafrika wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang ili kuchangisha pesa za kufanya wanachotaka kukifanya.
 
Palace wanaripotiwa kwamba wanahitaji Pauni 80 milioni ili waachane na Zaha, ambao wao wanamwona kuwa ni mchezaji wote bora zaidi. Lakini, shida inakuja sehemu moja tu kwamba Arsenal wameshindwa kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya na kufanya bajeti yao ya usajili kuwa finyu, Pauni 45 milioni tu.
 
Kwa mujibu wa BBC, kocha Unai Emery usajili muhimu anaotaka kwenye kikosi chake katika dirisha hili la majira ya kiangazi ni kumnasa Zaha, lakini atafanyaje wakati mmiliki Stan Kroenke hajatoa fungu la kutosha la usajili, basi ni kuuza mastaa tu.
 
Wachezaji wengine ukimweka kando Aubameyang ambao wanatajwa kwamba huenda wakapigwa bei ni Shkodran Mustafi na Mesut Ozil, huku kiungo Lucas Torreira naye akiwekwa kwenye mipango huyo baada ya kuwindwa na AC Milan ya Italia.
 
Manchester United, Arsenal, Manchester City na hata Liverpool kwa awamu tofauti wamekuwa wakiripotiwa kwamba wanafukuzia huduma ya winga huyo Muivory Coast, ambaye kwa sasa yupo na kikosi cha Tembo kwenye michuano ya Afcon 2019 huko Misri.
 
Hata hivyo, kuna taarifa mpya zinazodai kwamba Lille wamepigiwa simu na kuelezwa kwamba wasiwahesabie Liverpool kwenye mpango wa kumsajili staa wao huyo kwa sababu wakali hao wa Anfield hawana tena mpango wa kunasa saini ya Pepe.
 
Gezeti la Ufaransa la L’Equipe hivi karibuni lilifichua kwamba Inter Milan wameweka mezani ofa ya Pauni 72 milioni kwa ajili ya kunasa huduma ya Pepe ili akakipige kwenye kikosi chao huko Serie A msimu ujao.

Pepe ni moja ya mastaa ambao hawaonekani kama wataendelea kubaki kwenye timu zao wanazozitumikia kwa sasa kutokana na huduma zao walizoonyesha msimu uliopita kwenye ligi za nchi zao na hivyo kuwindwa na vigogo wa Ulaya kila kona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…