Kufahamu kurasa za tovuti fulani zilizoko kwenye Google
Ikiwa unataka kufahamu ni kurasa ngapi na zipi zimeorodheshwa au kutambulika (indexed) na Google katika tovuti fulani, unaweza kuandika “site:mfano.com” na utaona kurasa za tovuti yako.
Huduma hii ya Google ni muhimu sana kwa wenye tovuti na blogs kwani wataitumia kubaini ni kurasa zipi ambazo tayari Google imeshazitambua kutoka kwenye tovuti au blog zao.