Kampuni yatozwa Tsh. Bilioni 4 kwa kosa la kum-tag mrembo Kim Kardashian kwenye mtandao wa Instagram, Watumiaji wengine wapigwa onyo -------------------------------------------------------------------------------- Hakuna ubishi kwa sasa mtandao wa Instagram umekuwa chanzo kikubwa cha mapato kwa wasanii na watu wengine maarufu na ndio mtandao pekee wenye watumiaji hai (active users) wengi kwa hapa Tanzania. Ukweli ni kwamba mastaa wengi duniani kwa sasa wanaingioza pesa nyingi sana kupitia matangazo wanayoposti kwenye kurasa zao za Instagram. Na ukweli ni kwamba hata Makampuni makubwa yamekuwa yakiwatumia wasanii hao kutangaza bidhaa zao na yamekuwa yakiingiza faida kubwa kupitia matangazo hayo, Jambo ambalo linapelekea kwa sasa mtandao wa Instagram kuwa chanzo cha mapato kwa watu maarufu na hata wale wenye ‘page’ zenye wafuasi wengi. Sasa kufuatia ukweli huo, Kampuni moja ya mambo ya fasheni nchini Marekani iitwayo, Missguided imepigwa faini ya dola milioni $2.8 sawa na Tsh bilioni 4.2 kwa kosa la kumtag mwanamitindo Kim Kardashian na kutumia brand yake kibiashara. Kampuni hiyo inayotumia jina la missguided imekuwa ikim-tag Kim na kisha kueleza kuwa nguo hizo alizovaa zipo kwenye maduka yao