Mkuu mie hili suala la huyu musiba ndiyo limenimaliza kabisa kuona ni jinsi gani nchi yetu ilivyoharibika.
Pamoja na hao Kinana na Makamba kutokuwa watakatifu walichokifanya kuandika barua kuhusu huyo taahira musiba ni sawa kabisa.
Kilichonishangaza ni kuendelea kushambuliwa Kinana na Makamba na hao ambao waliomsukumia nduli na dikteta Ikulu Kikwete na Mkapa kuamua kuwa kimya kabisa. Mwinyi naye kuja juu kuhusu picha yake kutumika lakini kuona upuuzi kile kilichofanywa na hao wastaafu.
Hii nchi sijui kama itakuja kuwa sawa tena ninachokiona ni hali kuendelea kuwa mbaya zaidi na kuwepo chuki kubwa sana miongoni mwa Watanzania na maovu ya kutisha kuongezeka kwa kasi kubwa sana.