Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1557225659099.jpeg
 
Mwigizaji Wesley Snipes amewatoa hofu mashabiki wa filamu yake ya BLADE kuwa mwigizaji mpya wa filamu hio Mahershala Ali atafanya vizuri zaidi na watapata wanachotegemea kutoka kwa husika ya Blade 'muuaji wa Vampires'. - Wesley Snipes ameongea baada ya kupata habari za kushtukiza kuwa Marvel Cinematic Universe wametangaza ujio wa Blade mpya na yeye sio mwigizaji wa filamu hio nakusema 'Mashabiki tulieni, hii ndio biashara ya burudani ilivyo, amani kwa Marvel Cinematic Universe, mimi shabiki wenu kila wakati'. - Kuhusu muigizaji mpya wa Blade,Mahershala, Wesley Snipes anasema 'Hongera kwake, ni muigizaji mzuri na mwenye kipaje, nategemea kufanya nae kazi siku moja".
 
Bondia wa Urusi maxim dadashev amefariki dunia Marekani. Ni baada ya kumaliza pambano na bondia wa Puerto Rico Subriel Matias na kujeruhiwa vibaya kichwani. Mkufunzi wa bondia huyo aliyefariki akiwa na miaka 28 tu alikatisha pambano katika raundi ya 11. Baada ya kupitia picha za video mkufunzi huyo alionekana akimsihi Dadashev akubali kusitisha pambano baada ya kuona amepigwa sana. Hata hivyo baada ya kusitishwa bondia huyo alisaidiwa kutoka ulingoni kisha akaanza kutapika na kupoteza fahamu. Dadashev alifanyiwa upasuaji wa kichwa baada ya kuonekana damu imevuja kwenye ubongo. Amefariki akiwa na rekodi ya kushinda mapambano 13 na kupoteza pambano moja pekee.
 
Hakimu Mkuu Mkazi, Patrick Odhiambo amekonga nyoyo za watu wengi nchini Kenya baada ya kuchangisha fedha mahakamani za kumlipia Karyn Chelagat (19) aliyeshtakiwa kwa wizi wa nywele bandia, kisha akamuachia huru. Karyn alikiri kuiba nywele hizo ili naye apendeze kama rafiki zake. .
 
Mwanaume mmoja nchini Japan amesafiri 2,400km kumfuata mpenzi wake kwa ajili ya kum'surprise akiwa amevaa mdoli ulioziba uso, lakini akamkuta kakumbatiwa na mwanaume mwingine. Alipoondoka, mwanamke akamkimbilia na kumkumbatia. _ Raia wengi nchini Japan wamemsifia mwanaume huyo kwa moyo wake wa upendo. Unadhani ingekuwa kwako ingekuwaje?
 
SAID Stephen na mtoto wake wa kike (jina linahifadhiwa), wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Morogoro kwa tuhuma za kuhusika kwenye mauaji ya mtoto Greyson Valentino, aliyekuwa na umri wa mwaka mmoja na miezi saba. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).
 
Wilbroad Mutafungwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro leo tarehe 24 Julai 2019 amesema, maiti ya mtoto huyo imekutwa shambani kwa Said.
Mtoto wa Said mwenye umri wa miaka minane, anayesoma Darasa la Pili katika Shule ya Msingi Mpapa iliyopo wilayani Mvomero, anatuhumiwa kuhusika na mauaji hayo.
 
Taarifa zaidi zinaeleza, tukio hilo lilitokea tarehe 21 Julai 2019 mchana katika Kijiji cha Hembeti, Mvomero mkoani humo.
Siku ya tukio, Kamanda Valentino ameeleza kuwa baba wa marehemu alikuwa kanisani, na kuwa alipata taarifa ya mwanaye kupotea ndipo aliporejea nyumbani na kuanza kumtafuta.
 
Back
Top Bottom