Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1563970784508.jpeg
 
Kinda Joe Willock amejitengenezea mazingira mazuri ya kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal baada ya kuendelea kuonyesha kiwango bora kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Real Madrid jana Alfajiri,kama ilivyo kwa mshambuliaji Gareth Bale wa klabu hiyo ya Hispania.
 
Licha ya Arsenal kupoteza kwa mikwaju ya penati 3-2 baada ya timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2 kwenye muda wa kawaida, Willock (19) alitimiza vyema majukumu yake kwenye sehemu ya kiungo ya Arsenal, akimudu kupambana na wachezaji nyota na wenye majina makubwa wa Real Madrid katika dakika 45 alizocheza ikiwa ni siku tatu tangu alipofanya vizuri kwenye mechi dhidi ya Bayern Munich ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na msimu mpya.
 
Kiwango hicho bora cha Willock huenda kikalishawishi benchi la ufundi la Arsenal kumpa nafasi kinda huyo kwenye msimu ujao, hasa mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England dhidi ya Newcastle kutokana na nyota watatu wanaocheza nafasi ya kiungo wa kati, Mohamed Elneny, Lucas Torreira na Matteo Guendouzi kukosekana katika kipindi hiki cha kujiandaa na msimu.
 
Wakati Willock akitamba, nyota wa Real Madrid aliyeonyeshwa mlango wa kutokea, Gareth Bale naye aliendelea kumthibitishia kocha Zinedine Zidane kuwa anastahili kuendelea kubakia klabuni hapo kwa kufunga moja kati ya mabao mawili ya kiusawazisha ya Real Madrid kwenye mchezo huo.
 
Back
Top Bottom