Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1564211702558.jpeg
 
Reptilia na Amfibia
Hii ni sehemu muhimu zaidi kwa kuwa ina idadi kubwa ya wanyama kama nyoka, mijusi, vyura na wengine wengi wanaopatikana katika hifadhi hii tu. Kwa mazingira na hali ya hewa ya hifadhi hii ya Uduzungwa ndio inapelekea kuwepo kwa makazi na sehemu salama kabisa kwa wadudu wa aina mbali mbali ambo ni vigumu sana kuwaona sehemu nyingine.
 
Katika hifadhi hii hata mjusi na vyura wanahifadhiwa na kuchukuliwa kwa uzito kama vile wanyama wengine, hii ni hifadhi ya kipekee sana. Kwa utafiti uliofanyika hivi karibuni na watalaamu wa wanyama na wadudu, wamegundua aina za reptilia na amfibia ambao hawapatikani sehemu yoyote ile duniani isipokuwa hapa katika hifadhi ya Milima ya Uduzungwa.
 
Vipepeo
Kutokana na hali nzuri ya mazingira na miti ya maua mengi kwenye hifadhi hii, basi ndio pamekuwa ndio nyumbani kwa vipepeo wengi sana, ambao wanaifanya hifadhi hii kuvutia na kuwa na mwonekano mzuri. Vipepeo wanavutia sana na wana manufaa sana kwenye ikologia na utunzaji wa uasili wa uoto wa asili na mazingira. Ukitaka kuona vipepeo wengi mpaka ushangae tembelea hifadhi hii miezi ya Disembe mpaka Aprili au Mai.
 
Kwa utajiri na hali nzuri ya mazingira ya hifadhi hii ilitakiwa kuwa na idadi kubwa sana ya watalii au wageni, ndugu zangu watanzania haina haja ya kuwasubiria wageni kutoka Ulaya au Marekani ndio waanze kutembelea hifadhi hizi, tuanze sisi wenyewe kwa kuwa watalii wa ndani kwenye nchi yetu wenyewe. Hii ndi njia nzuri ya kuinua uchumi kwa nchi yetu. Ni jambo ambalo tunaliweza kabisa, ndio maana nimeamua kuandika makala hizi kwa lugha ya Kiswahili ili kuwahamasisha Watanzania kutembelea hifadhi za wanyama na vivutio vingine vilivyopo ndani ya nchi yetu.
 
Back
Top Bottom