Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1564211741923.jpeg
 
Katika kupandisha mlima huu wenye vilele viwili vya Lohomero urefu wa mita 2576 na Mwaniha urefu wa mita 2500, ambapo utakapo fika kileleni utaiona Morogoro nzima yani utashangaa mwenyewe, kwa hiyo kuna kutembea ili uweze kuona kila kinachoonekana kwenye hifadhi hii ya kipekee. Hakuna hifadhi nzuri kama hii jamani
 
Wageni wengi hupenda kupanda mlimani na wanaona ni sehemu yao nzuri ya kutembelea kwa sababu ya njia zake kupitika vizuri kabisa na bila kuathiri uoto, kila kitu kipo kwenye uasili wake kabisa. Zifuatazo ni njia ambazo mara nyingi hutumiwa na wageni wanapopanda kwenda kileleni mwa milima ya Uduzungwa,
 
Njia ya Sanjo ( Sanjo trail), ambayo ni kilomita 6 kwa muda wa masaa 3, kwenye njia hii kuna vivutio vingi sana kama, utakutana na wanyama jamii ya nyani, ndege wengi sana na mtakutana na maporomoko ya maji mara mbili, vile vile kwenye njia hii utakutana na uoto wa miti jamii ya miombo na miti mingine yenye kuvutia sana.
 
Sanje Circuit, ambayo ni umbali wa kilomita kama 5 na nusu ambapo mtatumia muda wa kama masaa manne, kwenye kutumia njia hii ya pili utakutana na vivitio vingi sana kama vile maporomoka madogo madogo 3, wanyama wengi jamii ya nyani na kima, vipepeo wengi sana na pia utaona uoto wa kipekee sana na wa kuvutia mnoo.
 
Prince Bernhard trail, hii ni njia ya yenye umbali wa kilomita moja, ambayo kwa kutembea utatumia kama dakika 40, vivutio unavyoweza kuviona kwenye njia hii ya tatu ni maporomoko madogo madogo, nyani wekundu, swala wa aina mbali mbali na ndege kwenye mlima Bokela.
 
Miti/ mimea
Kwa wale wanaopenda zaidi vivutio vya mimea ya aina mbali mbali yenye kuvutia kutokana na hali nzuri ya hewa basi hapa Uduzungwa ni sehemu yenyewe. Kwa wanaofanya utafiti kwenye miti au wanaojifunza kuhusu miti mbalimbali basi kwenye hifadhi hii ni sehemu ya kufikiria kwenda kufanya hivyo. Eneo hili la hifadhi ya milima ya Uduzungwa lina aina na jamii nyigi sana za miti na mimea mbali mbali zaidi ya 2500, ambayo kati ya hiyo 160 ni miti ya dawa mbali mbali. Hifadhi hii inayosifika kwa kuwa na miti migi ya dawa zenye kutibu maradhi na magojwa mbali mbali. Hivyo panga kutembelea hifadhi hii maridhawa kabisa.
 
Sehemu nzuri ya kuwaona ndege (bird watching)
Hifadhi hii inasifika Afrika na duniani kote kama sehemu yenye aina nyingi za ndege, hifadhi ya Milima ya Uduzungwa ni ya pili kwa Afrika kwa kuwa na idadi kubwa sana ya ndege. Na pia hifadhi hii ni muhimu zaidi kwa wale wanaopenda ndege au kujifunza kuhusu ndege, kuna aina zaidi ya 250 ya ndege ambao wanapatikana hapa kwenye hifadhi hii tu, na hawapaikani sehemu nyinge.
 
Back
Top Bottom