Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1564319961563.jpeg
 
Ni wazi kuwa, ulimwengu wa intaneti wa leo ulianzwa na mwanasayansi wa kompyuta wa Uingereza Tim Berners-Lee. Kuundwa kwa intaneti yake ya kwanza, moja kwa moja kulibadili ulimwengu, vyombo vya habari, mahusiano, burudani na mambo mengine mengi.

Tunapotazama intaneti leo, ni wazi kuwa tunaona mambo mengi ambayo intaneti imepitia tokea kuanzishwa kwake hadi hivi leo. Karibu ufuatilie makala hii ili ufahamu mambo 18 ya kushangaza kuhusu intaneti usiyoyajua.
 
Takriban barua pepe bilioni 247 hutumwa kwa siku

Kampuni ya Radicati inakadiria kuwa takriban barua pepe bilioni 247 hutumwa kila siku. Inaelezwa kuwa asilimia 90 ya barua pepe hizo ni barua pepe hatarishi (SPAM) na Virusi, hivyo kuwa makini na barua pepe unazofungua.
 
Tweet ya kwanza ilichapishwa Machi 21, 2006 na Jack Dorsey

Nani alifahamu kuwa Twitter ingekuwa maarufu duniani kama ilivyo leo? Mnamo Machi 21, 2006 Jack Dorsey aliandika tweet ya kwanza iliyokuwa inasema, “Just setting up my twttr.” lakini hivi leo Twitter imeshakuwa na mamilioni ya watumiaji ulimwenguni kote.
 
Video iliyotazamwa kuliko zote kwenye mtandao ni Despacito

Wimbo wa Despacito ulioimbwa na Luis Fonsi na Daddy Yankee ni wimbo unaoongoza kwa kutazamwa na watu wengi zaidi kwenye mtandao wa YouTube. Wimbo huu umeshatazamwa mara bilioni 3.55 hadi sasa.
 
Saa 300 za video hupakiwa kila dakika kwenye YouTube

YouTube ni mtandao maarufu ambao wengi wanaufahamu kama mtandao wa kusambaza na kutazama video kwenye mtandao. Lakini je unajua kuwa kwa muda wa dakika moja video zenye jumla ya urefu wa saa 300 hupakiwa katika mtandao huu? Tovuti hii hupokea video kutoka kwa watumiaji mbalimbali duniani kote
 
Back
Top Bottom