Bendi yangu ilikuwa inaitwa Bambino Sound, ambayo ilidumu kwa miezi kadhaa tu, lakini ilivunjika kutokana na kutokuwa na uongozi mzuri, haikuwa na mtu makini hilo ndilo liliangusha bendi hii, hatimae nikarudi tena African Stars Band. Baadaye nilienda Extra Bongo…” alisema Banza katika mahojiano wakati wa uhai wake.
Bendi hiyo haikudumu kwa kipindi kirefu, ikafa.
Banza Stone alikuwa , mtunzi, mwimbaji na rapa wa muziki huo nchini. Pia alianika idadi ya bendi alizopitia katika kipindi cha miaka 23 tangu aanze muziki wa dansi rasmi.Aliweka wazi kwamba alipita kupiga muziki katika bendi zaidi ya bendi tisa, katika harakati zake za za muziki.