Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mkondo wa bahari wa Hormuz bado ndio njia bora ya kusafirisha kiwango kikubwa cha mafuta kutoka eneo la Ghuba na njia pekee kupitia baharini.
Kuna njia za ardhini ambazo pia hutumika kusafirisha mafuta kutoka eneo la Ghuba.
Bomba la mafuta la Saudia linaelekea katika bahari nyekundu , na lina kiwango cha mapipa milioni tano ya mafuta kwa siku.
 
Abu Dhabi nayo ina bomba la mafuta ambalo hubeba takriban mapipa milioni 1.5 ya mafuta kwa siku katika pwani yake na kusafirisha mbele ya mkondo wa Hormuz.
Na kuna bomba jingine la mafuta linaloweza kusafirisha mafuta ya Iraq hadi pwani ya Mediterenean.
Lakini sio kwamba mabomba haya ya mafuta yanafanya kazi asilimia 100.
Na hayawezi kusafirisha kiwango kikubwa cha mafuta kama kile kinachosafirishwa na meli.
 
Sheria za Umoja wa mataifa zinaruhusu mataifa yote kudhibiti maili 13.8 kutoka kwa pwani yake.
Hiyo inamaanisha kwamba eneo jembamba zaidi la mkondo huo lipo kati ya Iran na mji wa Oman.
Iran huruhusiwa kuendeleza shughuli zake katika maji yake - lakini sio kuathiri safari za meli nyengine za kigeni.
 
Marekani sasa imeimarisha uwepo wa jeshi lake katika eneo hilo.
Lakini imesema kuwa ni vyema kwa mataifa mengine kufanya juhudi za kuimarisha usalama katika eneo la Ghuba na eneo zima kwa jumla.
Na Uingereza imetoa meli ambazo zitaweka usalama katika mkondo wa Hormuz.
 
City imemlenga mchezaji wa kiungo cha mbele wa Real Sociedad mwenye umri wa miaka 22 Mikel Oyarzabal kama mchezaji atakayeichukua nafasi ya Sane na wapo tayari kulipa kitita cha Euro milioni 75 zinazohitajika kw a mujibu wa mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania ili kuachiliwa. (AS)
 
Perez, mwenye umri wa miaka 72, aliamua kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Tottenham mwenye miaka 30, ana thamani kubwa mno kuchukuliwa kwa urahisi huku Jiangsu Suning ikitarajiwa kumsajili katika uhamisho wa bure. (Daily Star)
 
Winga wa Lille Nicolas Pepe, mwenye miaka 24, atakamilisha uhamisho wake wa thamani ya £72m kwenda Arsenal Jumanne au Jumatano -ili mradi mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain hawatojaribu kuteka makubaliano hayo. (La Voix Du Nord)
 
Everton imewasilisha ombi la £55m pesa taslimu kumsajili mchezaji wa kiungo cha mbele wa Crystal Palace Wilfried Zaha huku kukiwa hakuna mchezaji wanayejitolea kubadilishana na wapinzani wao katika Premier League. (Sky Sports)
 
Palace inataka £60m awali ili kumuachia mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast na pia ina wasiwasi kuhusu namna Everton inavyotaka kupangia malipo katika makubaliano yoyote yanayowezekana kuidhinishwa. (Daily Mirror)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…