Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kipindi cha mchezo cha Daniel kufikia sasa: Alianza kuichezea rasmi AC Milan wiki hii katika mechi ya kirafiki dhidi ya Bayern Munich.
Cha kushangaza: Jezi nambari tatu iliofanywa maarufu na Paolo ilistaafishwa wakati Maldini alipostaafu lakini ameiruhusu klabu hiyo kuitumia tena iwapo mwanae ataichezea klabu hiyo.
 
Justin Kluivert - 20, Roma
Patrick Kluivert aliichezea miamba ya Ajax, AC Milan na Barcelona wakati wa kipindi chake cha mchezo ambapo alifunga magoli 205.
Katika mechi 79 akiichezea Uholanzi alifunga magoli 40 na kuwasaidia katika nusu fainali ya kombe la dunia 1998.
 
Alishinda mataji machache, ikiwemo lile la Eredivise mara mbili, La Liga na lile la klabu ya mabingwa ambapo alifunga goli la ushindi wakati alipokuwa na umri wa miaka 18.
Kipindi cha mchezo wa Justina kufikia sasa: Yeye pia alianza kuichezea Ajax na kufunga goli lake la kwanza miaka kumi na siku moja tangu babake kufunga goli lake la mwisho.
 
Pia alishinda medali ya nafasi ya pili ya Ulaya katika kipindi cha mwaka 2016/17. Kama babake, alielekea Itali baada ya kusainiwa na klabu ya Roma mwaka 2018.
Ijapokuwa anajaribu kuingia katika kikosi cha kwanza cha timu alikuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi wa Roma kufunga goli katika ligi ya mabingwa msimu uliopita baada ya kufunga dhidi ya Viktoria Plzen, likiwa bao lake la kwanza la klabu hiyo.
 
Hahahahaha, badili mkuu ufaudu Pa...chi za halali ujiepushe na michepuko.
Ulitaka kimbau mbau, utakuwa naye, ukitaka tipwatipwa utasogeza, ukimtaka mweupe, mweusi, mfupi, mrefu utajipatia tu .
Kazi kwako Kamanda[emoji23]
Kabisa yaani. Majimama yenye mamisambwanda ya kufa mtu matatu - mawili meupe marefu na limoja jeusi tii kimo cha kati; na kakimbaumbau kamoja ka kuchangamsha familia. Paradise on Earth indeed wallahi. Ngoja nianze tuisheni ya Kiarabu kwanza asubuhi na mapema. Process za kusilimu zikoje kamanda? [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Babake alikuwa Mwafrika wa kwanza kushinda taji la Ballon d'Or. Kwa sasa ndiye rais wa taifa la Liberia.
Goerge Weah alijitengenezea jina lake nchini Ufaransa wakati aliposajiliwa na Arsene Wenger kutoka Monaco kwa dau la £12,000.
 
Alikuwa mchezaji maarufu duniani nchini Italy na kuisadia AC Milan kushinda mataji mawili ya ligi , Ballon D'Or na kufunga goli maarufu ambapo alitamba na mpira kutoka upande mmoja wa kiwanja na kuwachenga karibia wacheza wote wa klabu ya Hellas Verona kabla ya kufunga.
 
Kipindi cha mchezo wa Timothy kufikia sasa: Akianza kusakata soka katika klabu ya New York red Bull , mchezaji huyo wa Marekani alifuata nyanyo za babake akitia saini kandarasi yake ya kwanza na klabu ya PSG.
Ni wazi kwamba ingekuwa vigumu kubeba jina lake huku timu hiyo ikiwa na wachezaji maarufu kama vile Neymar, Kylian Mbappe na Edinson Cavani.
 
Akiwa maradona wa Carpathians' {mlima mmoja nchini Romania ) Gheorghe Hagi - ni mchezaji nyota aliyeichezea Real Madrid, Barcelona na Galatasaray - alitajwa kuwa mojawapo ya wachezaji wazuri zaidi duniani katika miaka 80 na 90.
Kiungo huyo mshambuliaji alicheza mara 125 na ametajwa kuwa mchezaji bora nchini Romania.
 
Mchezo wa Ian kufikia sasa: Akichaguliwa mara mbili kama mshindi wa tuzo ya Golden Boy, talanta yake imeonekana.
Alianza kucheza soka katika taasisi ilioanzishwa na babake na baadaye ikafunzwa na Gheorghe huko Viitorul Constanta.
 
Ijapokuwa uhamisho wake kutoka Romania hadi Fiorentina haukufanya kazi, Ian alijipatia matumaini katika klabu ya Viitorul kabla ya kuelekea klabu ya Genk nchini Ubelgiji - klabu ambayo ilizindua mchezo wa Kevin De Bryune, Divock Origi na Thibaut Courtois.
Cha kushangaza: Babake alimfanya nahodha wa klabu ya Viitorul Constanta akiwa na umri wa miaka 20.
 
Luca Zidane - 21, Racing Club Santander ( kwa mkopo)
Luca Zidane - 21, Racing Club Santander (on loan)
Kuwa Zinedine Zidane - mmoja ya wachezaji bora zaidi duniani , alieshinda kila kitu ambacho mchezaji na mkufunzi alitaka kushinda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…