Very true kuna mdada mmoja humu jina kapuni. Misimamo yetu kwenye lile jukwaaumiza kichwa inashabihiana sana. Mwisho tukaanza kuchat kule pm. Akanambia jinsi ambavyo ofisini kwake jina kapuni ninavyopendwa na colleagues wake wengi kuhusu michango yangu kule siasani na mdada mmoja yeye anakusanya nyimbo zote humu zinazowekwa na BAK, nilishangaa sana kusema kweli. Akaendelea kuniambia kama siku nikifika ofisini kwake halafu awaambie colleagues BAK yuko hapa alidai kazi siku hiyo hazifanyika hata chembe. Mie kule siasani natetea tu maslahi ya nchi yetu na uhuru na haki ya Watanzania kumchagua mtu tunayemtaka kuongoza nchi yetu awe wa Chadema, ccm or ACT na siasa wala siipendi hata chembe, kama naye atavurunda basi uchaguzi mwingine ataondolewa kwa nguvu ya kura. Kumbe kwa kuyasimamia hayo kuna wengine unawagusa kupitiliza.