Gwiji mwingine wa Chelsea, Frank Lampard, amerejea klabuni hapo akiwa kocha mkuu wa timu ya wakubwa.
Hakuna kati ya watatu hao mwenye uzoefu na nafasi aliyopewa kwenye Ligi Kuu, ingawa Lampard alikuwa kocha wa Derby County katika Ligi Daraja la Kwanza msimu uliopita, akiwafikisha kwenye fainali ya mechi za ‘playoff’ ambako walifungwa dhidi ya Aston Villa waliopanda Ligi Kuu wa England.
Makelele aliwahi kufanya kazi katika benchi la ufundi la PSG baada ya kustaafu soka 2011.
Akawa kocha msaidizi PSG 2011-13 chini ya Paul Clement. Kisha akawa kocha mkuu wa Bastia kwa msimu mmoja 2014.