Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

WAFAHAMU WANYAMA WANAOCHANJA MBUGA (MBIO)
Leo nimeona si mbaya kama nitakuletea habari ya viumbe hai ambao wanaspidi kubwa huko hifadhini, ili siku ukijichanganya ukaingia kwenye kumi na nane zao, yakitokea yakutokea ujue unakimbizwa na nani na uwezo wake kukimbia ukoje, kama nilivyo huwa nakuletea mambo live kutoka mbuga zetu tuu yaani Serengeti, mikumi, ngorongoro, katavi, kutulo, ruaha nk, hivyo sitegemei utamuona mnyama kama kangaroo au wolf japokuwa nao ni kiboko katika mbio lakini kwa bahati mbaya hapa kwetu hao jamaa hawapo kabisa, baada ya utangulizi huo naomba sasa nianze na list yangu.
 
Chui
Moja kati ya viumbe niliowahi kuwachambua kama utatizama katika ukurasa huu ni chui, nilikueleza sifa yake kubwa huyu kiumbe ni kwamba ana aibu sana, hamuwezi tizamana usoni na ukilazimisha jambo hilo basi yeye huwa anajifanya eti kalala usingizi, nilikueleza pia ni mjanja mjanja na muongo, ukitaka kujua hilo sikia hii, anapokuwa na njaa aibu zake huweka kando kwani mbuga nzima yeye ndio bigwa wa riadhaa ana uwezo wa kukimbia 120 km kwa kutumia saa moja tuu.
 
Swala.
Mnyama pekee anayeishi pasina amani sababu ya unyonge wake, swala hata sungura akipita katikati ya miguu yake yeye huwa anaruka juu, kwakuwa anajua tayari kumekucha, hupendelea kukaa jilani na wanyama wababe kwa sababu ya usalama wake mfano tembo, twiga na nyati, pamoja na unyonge wake lakini mbio tuu alipewa, anaweza kimbia kwa spidi moja na chui na wakati mwingine akamshinda lakini chui akimkomalia atamkamataa tuu kwakuwa kenyewe huwai kuchoka, anauwezo wa kukimbia km 88 kwa saa.
 
Swala.
Mnyama pekee anayeishi pasina amani sababu ya unyonge wake, swala hata sungura akipita katikati ya miguu yake yeye huwa anaruka juu, kwakuwa anajua tayari kumekucha, hupendelea kukaa jilani na wanyama wababe kwa sababu ya usalama wake mfano tembo, twiga na nyati, pamoja na unyonge wake lakini mbio tuu alipewa, anaweza kimbia kwa spidi moja na chui na wakati mwingine akamshinda lakini chui akimkomalia atamkamataa tuu kwakuwa kenyewe huwai kuchoka, anauwezo wa kukimbia km 88 kwa saa.
 
Simba na Nyumbu
Kama ungekuwa mtihani basi tungesema hawa wawili wamegongana, nyumbu ndio mnyama mjinga porini kati ya wanyama wenye miili mikubwa, anaweza akawa anakula majani na akajiuliza kwanini sikimbii na akaanza kukimbia, na wakati anakimbia akajiuliza kwanini nakimbia akaacha kukimbia, ni wanyama ambao maamuzi yao hufanyika pasina utaratibu na pasina ulazima wa kufanya hivyo, wakati upande wa simba ni mnyama ambaye hujipanga kabla ya kufanya jambo lolote, hawa jamaa wana uwezo sawa katika mbio, sababu kuu ambayo hufanya simba kuwakamata kiurahisi ni kwa sababu huwawinda kwa akili sana lakini kwa kesi ya mbio wasijemsingizia mtu na simba wote hukimbia km 80.5 kwa saa moja.
 
Mbwa Mwitu.
Ukiwaona huwezi kuwazania ni wanyama wadogo sana wanaokula nyama na wawindaji, katika umbo hata fisi ni mkubwa kwao, wana heshima kubwa hawa jamaa si fisi wala simba huwa wanawaheshimu, wakiwa na nyama wanawaachia bila shuruti, ubabe wao huwa kwakuwa wanatembea kwa makundi makubwa kama vibaka wa panya road, maisha yao ni mpera mpela usikosee ukapita jilani yao una damu umekwisha, hawapatani na damu kabisa wakiiona tuu majini yao huamka, hata mwenzao wanaweza kumla, vidogo vina nguvu, wakati mwingine huangusha hata wanyama wakubwa, tabia yao ni kung’ata akitoka na nyama anakula kisha anafuta mdomo anarudi tena kuifata, sifa yao nyingine ni mbio wanauwezo wa kukimbia umbali wa km 71 kwa saa moja tuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…