Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Pundamilia
Ni mnyama anayekula majani tuu, msafi na mrembo ana ngozi yenye kuvutia inayonakishiwa na mistari mieupe na mieusi, anapiga sana mateke unapokutana na simba mdomo umepinda we jua tuu muhusika anaweza kuwa pundamilia, kama farasi angelikuwa ni mnyama wa polini basi angekuwa juu ya pundamilia kwani wakati farasi akimaliza km 70 kwa saa, pundamilia hutumia saa moja kwa km 64.
 
FISI
Al maarufu kama bwana afya, pamoja na kuwa na miguu mifupi ya nyuma, lakini huyu jamaa huenda akawa ndio miongoni mwa wanyama wawindaji ambao wanashika mkia kwa spid ndogo, sifa yake ya kipekee yeye huweza kukimbia umbali mrefu kwa taratibu, lakini akiamua kufunguka njaa inapotaka kuzidi viwango, huweza kutumia saa moja kwa km 60, ila ni nadra sana kumuona akifanya hivyo kwakuwa amezoea vitu laini laini tuu, kama uporaji na kujitafutia mizoga pamoja na mifupa.
Nafikiri hata nikiishia hapa si mbaya kwakuwa nitakuwa nimekupa mwanga kidogo, sababu ya kuukata uzi huu hapa ni hivi anayeweza kufuata baada ya fisi kwa mbio ni mwanadamu, akina Bolt wanaiweza michezo hiyo, kikubwa cha tofauti kwa wanadamu ni kuwa hutofautiana kwa kiasi kikubwa katika kukimbia, tofauti na wanyama ambao kwa kiasi kikubwa hufanana.
 
kwa wale ambao watakuwa hawaelewi km zikoje ngoja nikufafanulie km 1 sawa sawa na mita 1000, na mita 1000 ni sawa na viwanja kumi vya mpira wa miguu uviunganishe, kama bado hujanielewa sikia na hii umbali wa kutoka Dsm mpaka mbeya ni km 880, na Dsm to Mwanza ni 1200, hivyo kusingekuwa kuchoka chui alikuwa na uwezo wa kutoka Dsm mpaka Mwanza kwa saa 10 tuu, na kwa swala pia angetumia saa 10 kutoka Dsm kwenda mbeya, bahati mbaya cc zao si za kupasua anga hizo, hebu mwacheni Mungu aitwe Mungu, kwa maajabu haya unafikili umebakiza nini kwenda mbugani kuwatizama hawa JAMAAA.
 
Hadithi ya kusikitisha.

Jumping into conclusions...

Wana kawaida hiyo ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…