Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani ya mwili Dk. Meshack Shimwela amesema zipo sababu tofauti zinazosababisha vifo vya ghafla, baadhi ikiwa ni maradhi ya moyo, mapafu, ubongo, mfumo wa upumuaji na wakati mwingine sumu.
 
Mara nyingi sababu kuu huwa ni matatizo katika mishipa inayopeleka damu katika misuli ya moyo mishipa hiyo huathirika kutokana na urundikaji wa lehemu mwilini hivyo kusababisha mishipa hiyo kunyauka na kukakamaa hivyo kuifanya ishindwe kutanuka na kuwa myembamba.
 
Vilevile, damu iliyoganda nakuwa kama vibuja vya ugali huweza kutoka sehemu yoyote ya mwili kupitia mzunguko wa damu hufika katika mishipa inayopeleka damu safi katika misuli ya moyo na kuwa kizuizi cha damu kupita, hivyo basi mambo haya matatu yakitokea husababisha misuli ya moyo kukosa damu kabisa ua kupata kiasi kidogo sana.
 
Anaeleza kuwa sababu ya pili ni misuli ya chumba cha upande wa kushoto wa moyo kuongezeka ukubwa na mara nyingi huwapata wenye shinikizo la damu la muda mrefu hii ni kutokana na kujibadili kwa misuli ya moyo na kuongezeka ukubwa na kufanya kazi ya ziada ya kusukuma damu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…