Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wee mzee [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Habari, naomba ushauri wako, mimi ni Mama wa miaka 42, nimeolewa na ndoa yangu ina miaka 14 sasa, sina tatizo la kindoa mimi na mume wangu tuko vizuri sana. Sababu ya kuja kwako nikuwa, mimi nina mdogo wangu ambaye ni marehemu sasa. Tulikua tuko karibu na alikua na pesa zake, alikua ananipenda na kunishirikisha kwa kila kitu chake, pia nina ndugu wengine watatu, mmoja ni mdogo bado yupo chuo na wengine wana familia zao. Marehemu baada ya kuoa kuna kipindi alikua haelewani na mke wake ili kujilinda tulimshauri vitu vyake awe anandika majina ya Mama lli kama ikitokea wataachana basi mke wake asichukue chochote. Kwakua Kaka alikua ni muelewa basi alifanya hivyo, alikua na nyumba akaandika jina la Mama na viwanja vingine. Kwa bahati mbaya Mdogo wangu alifariki mwaka jana mwishoni na kucha watoto wawili. Katika mirathi walitaka kumpa nyumba mke wake ndipo mimi na ndugu zangu tukasimama kidete kuwa nyumba si ya marehemu kwani ilikua na jina la Mama, ilileta utata mwanamke akitaka achukue nyumba lakini mwisho tulishinda na mali za marehemu ndugu yetu zikabaki kwa Mama kama mmiliki halali. Mwanzo Mama likua hajui kama kaka kaandika majina yake kwenye nyumba na viwanja vyake, lakini baada ya kujua hakusema chochote. Lakini baada ya kumaliza mambo ya mirathi Mama alisema kuwa mke wa marehemu abaki kwenye nyumba ile alee watoto. Sisi hatukua na shida kwani tulijua mwisho wa siku zitarudi kwetu. Tatizo mpaka sasa kuja kwako nikuwa Mama anataka kubadilisha majina ya mali za marehemu Kaka, anataka kuandika majina ya wajukuu zake ambao ni watoto wa marehemu kwa madai kuwa kama akifa hawatapata kitu. Shida nikuwa watoto wanakaa na Mama yao inamaana akishawapa kwakua ni wadogo yeye ndiyo atasimamia, tumamuambia Mama hata kama anaandika basi ateue ndugu kuzisimamia lakini hataki anasema mali ni zake anaamua mwewnyewe azifanyie nini? Kisheria ni zake lakini sisi ni watoto wake na wote hatukubaliani kwani kama Kaka hakumuamini mke wake akamuchia mali kwanini Mama amuamini, je sisi kama watoto tunaweza kufanya nini ili kuzuia mali za ndugu yetu zisipotee?
 
Naomba ushauri, wakati nakutana na huyu Kaka aliniambia wazi kuwa ana watoto wawili na wote amezaa na Mama tofauti na kuniambia kuwa wameachana na Mama wa watoto wake. Tulianzisha mahusiano lakini alikua ni msiri sana, hakutaka nijue anapoishi, kila nikimuambia anipeleke kwake alikua akizuga mara kwangu sijui nyumba ya kupanga, subiri nijenge kwangu ndiyo nitakupeleka, na maneno mengi mpaka nikawa siulizi tena. Nilifanikiwa kupata ujauzito wa kwanza, nikamuambia aje kwetu kujitambulisha lakini aliniambia kuwa nisubiri, mpaka najifungua hakuja kwetu Zaidi ya kuongea tu na ndugu zangu, nilipobeba ujauzito wa pili nilikomaa mpaka akaja nyumbani kwetu, akajitambulisha lakini hakurudi tena. Kwakua nilikua na watoto naye nilimlazimisha mpaka akanunua kiwanja, tulifanikiwa tukajenga, sikuchangia sana kwenye ujenzi lakini nilikua nahudumia familia na pesa yake alikua anapeleka kujenga. Kumbuka hatukua tukiishi pamoja kwani alikataa akiniambia kuwa anataka mpaka ndoa ingawa mara nyingi alikua anakuja na kukaa kwangu anaondoka. Sababu ya kuja kwako nikuwa, tangu mwaka jana nyumba aliyokua anajenga iliisha, nilikua namuambia tuhamie anakataa anasema nisubiri mpaka ndoa ndiyo tutahamia, alinikataza kabisa kwenda na alifunga mageti, lakini wiki iliyopita niliamua kwenda kuangalia, nilipofika nikamkuta mmoja wa wanawake aliozaa naye anaishi pale na mtoto wake na tena ana ujauzito mwingine. Nilipomuuliza ananiambia kuwa wote sisi ni wake zake anaweza kutuoa wote au akachagua mmoja hajafanya maamuzi bado hivyo nisipaniki. Kaka nimechanganyikiwa sijui nifanye nini? Kumpenda bado nampenda lakini nawaza mwanzo aliniambia huyo mwanamke yuko kwao Kigoma lakini nashangaa kamleta Dar na anaishi katika nyumba ambayo mimi nimchangia kujenga kwa kiasi kikubwa sana! Kuna mapenzi kweli hapa kaka au ananipotezea muda tu, anasema hawezi kuniacha kwani nina akili sana na namsaidia mambo yake je ananipenda au anataka tu kunitumia?
 
Kabla ya kufunga ndoa na mke wangu wa sasa kuna mwanamke niliishi naye miaka 8, Mungu alitujaalia watoto wawili, lakini nilishindwana naye tukaachana na kila mtu akashika njia yake. Kutokana na hasira tu za kuachana naye na mke wangu kutokutaka niwasiliane naye basi nilikaya mawasiliano kwa miaka minne sikujua anaendeleaje. Lakini mwaka jana kwa bahati mbaya alifariki kwa ajali ya gari na kwakua nina watoto naye ndugu zake waliniambia ingawa sikua na mawasiliano nao. Nilienda nikazika na kuamua kuwachukua wanangu, mwanzo ndugu zake walikataa kwa madai kuwa nilikua sihudumii chochote kipindi nimeachana na marehemu. Lakini nilipambana mpaka ustawi wa jamii nikawapata wanangu. Lakini sasa hivi tatizo linakuja kwenye mali, X wangu aliacha mali ambazo mimi naamini sasa hivi ni kwaajili ya wanangu, aliacha nyumba mbili na magari mawili na pia aliacha duka. Sasa tatizo nikuwa ndugu zake wamezing’ang’ania kuwa zitabaki watasimamia wao mpaka watoto wafikie umri wa kuzimiliki. Wanalipa ada sawa lakini hawa ni wanangu, mali za Mama yao ni kama zangu tu kwani mimi ndiyo nawasimamia, kwanini watoto waendelee kubanana kwenye nyumba ya kupanga wakati Mama yao ana nyumba tena mbili. Naomba ushauri wako, ni kwa namna gani ninaweza kupata haki za wanangu mimi kama Baba yao, najua Mama yao alichuma kwajili ya wanae na si kuziacha kutumiwa na ndugu zake ambao hata hawajui uchungu wa mtoto, naomba ushauri nifanye nini kwani naona wanangu kama wanateseka wakati mali zipo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…