Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mitaa ya hovyo hiyo usiende bro...

Mbali na kujiunganisha kwenye gridi ya taifa, sasa kuna hili jingine sugu aisee halisikii dawa. Antibayotikisi zote zinabaunsi tu na linaua watu balaa na kusababisha ugumba hata kwa wanaobahatisha kupona...
Ni hatari sana bro...siwezi pitia hiyo mitaa bro[emoji120]
 
Sukari ni moja katika familia ya Carbohydrates.
Carbohydrates ndio chanzo kikuu cha nguvu katika miili yetu. Hata hivyo, sio kwamba carbohydrates zote zinaweza kunyonywa au kutumiwa na miili yetu kama ilivyo. Kabla ya kuendelea hebu tuangalie aina za carbohydrates.
 
Carbohydrates ina aina kuu tatu, Monosaccharides, Disaccharides na Polysaccharides.
Monosaccharides kwa jina lingine hujulikana kama sukari rahisi (simple sugar) ambayo humeng’enywa moja kwa moja bila ya kuvunjwa vunjwa katika mfumo wa mmeng’enyo.
 
Ile sukari ambayo bado haijabadilishwa au kuvunjwa kwa jina lingine hujulikana kama Glycogen
Glycogen huhifadhiwa katika ini na misuli na hii hutokea ikiwa glucose imezidi mwilini hivyo hubadilishwa kuwa Glycogen na kuhifadhiwa katika ini na misuli
 
Inabidi pia ijulikane kuwa sio kwamba tu sukari tunayokula ndiyo huongeza sukari mwilini Lakini wanga pia huongeza sukari mwilini ambayo kwa mwanzo wakati unaila huwezi kuhisi utamu hata mara moja, Lakini ikishameng’enywa hubadilishwa katika sukari na kuongeza sukari katika damu.
 
Ikiwa Glucose itazidi mwilini, basi sehemu ya Glucose hubadilishwa kurudi katika Polysaccharides (Glycogen) na kuhifadhiwa katika ini na misuli. Ikiwa Glucose itapungua sasa, ndipo ile Glycogen iliyohifadhiwa katika ini itakapobadilishwa kuwa Glucose na kuendelea kufanya kazi yake.
 
Kongosho (Pancreas) ni organ inayotoa homoni ya Insulin, insulin ni homoni ambayo kazi yake kubwa ni kudhibiti kiwango cha sukari mwilini, kama kiwango kikizidi basi hupunguza mpaka idadi yake inayohitajika, na kama ikipungua basi hurekebisha mpaka kufikia idadi yake inayohitajika mwilini.
 
Back
Top Bottom