Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kutoelewa Msaada Unaohitaji ili Kuendesha Biashara Yako



Biashara ya mtandaoni ni kubwa. Na kama unaamua kuingia kuifanya, basi ni vema kujua ni msaada . Kama unaamua kufungua tovuti na mitandao ya kijamii kwa ajili ya biashara yako, tafuta mtaalamu wa kukusaidia. Kama unaona hautaweza kuendesha mitandao ya kijamii peke yako, tafuta mtu wa kukusaidia. Ni vigumu kufanya kila kitu kuanzia kuhudumia wateja (wanaopiga simu na wanaotuma meseji kwenye mitandao ya kijamii), kufanya mauzo na matangazo n.k
 
Kama umeamua kuwekeza katika biashara ya mtandaoni, basi ni vyema pia kutenga bajeti kwa ajili ya rasilimali watu. Unaweza kuandaa fungu kwa ajili ya watu watakaokusaidia katika kuunda na kuendesha mitandao yako. Kufanya hivi kunaweza kukusaidia kushughulikia mambo yale ambayo yanaweza kukuza biashara yako
 
Kushindwa Kutoa Kipaumbele kwa Huduma kwa Wateja

Kosa kubwa linalofanywa wakati wa kuanzisha biashara ya mtandaoni ni kuweka bidhaa bila kujali huduma kwa wateja.. Kwa mazingira ya Kitanzania ambapo bado wateja wengi wana wasiwasi na masoko ya mtandaoni kwa ukionyesha dalili yeyote ya kushindwa kumridhisha basi unaweza kumkosa.
 
Kama unauza vitu mtandaoni, ni muhimu kujua nje ndani juu ya bidhaa yako. Unaweza ukawauzia watu kitu au huduma na maswali yakawa mengi juu ya matumizi. Kama utashindwa kujibu utaonekana mbabaishaji. Jifunze kila kitu kuhusu bidhaa yako, maswali wanayoweza kukuuliza, changamoto n.k. Itakuwa rahisi sana wakipiga simu kuuliza maswali utaweza kuwasaidia. Hii itawatengenezea moyo wa kukuamini na kukutegemea. Mara nyingine wakitaka kitu/huduma, lazima wagonge mlango wako
 
Kutokuwa Na Mkakati wa Kutangaza Biashara



Kama mmiliki wa biashara, kuwa na mkakati madhubuti wa kuitangaza na kuuza bia shara. Haijalishi unauza nini, ni lazima ujifunze na ujue namna na mahala pa kupata wanunuzi wa bidhaa yako.
 
Pia wauzaji wengi hawapuzii vitu kama punguzo la bei, nafasi ya kujifunza kutokana na takwimu za mitandao ya kijamii. Pia, kuwa na tovuti inayowezesha wanunuzi kukufikia au kufanya malipo kwa urahisi ili kupata bidhaa wanazotaka ni moja ya njia nzuri ya kuongeza wateja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…