"Hakimu tangu nimefika hapa wanahabari wamekazana kunipiga picha, mpaka naingia humu ndani wananipiga picha tu bila kujua kwenye akili yangu nawaza nini, kwa sasa kichwa changu kimechanganyikiwa sana, hata hii kesi yenyewe sielewi itakuwaje. "Nimekaa nitulize akili yangu, wanahabari wananisogelea sogelea kunipiga picha, wananivua hadi kofia ili wanipige picha, mimi sijapenda, sasa nitakuja kuishangaza Mahakama, nitafanya jambo ambalo si la kawaida." - Mtuhumiwa Hamis Luwongo, anayetuhumiwa kwa mauaji ya mkewe, Naomi Marijani.