Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wakati mwa mwezi wa Ramadhan — Waislam wote ulimwenguni huungana kutimiza ibada ya mwezi wa 9 katika kalenda ya Kiislam, kama mwezi wa kufunga. Ni muhimu kwa watu wote wanaoshiriki kufunga mwezi huu, kuzingatia na kudumisha afya na lishe wakati wa kutekeleza ibada hii. Hizi ni baadhi ya dondoo zitakazokuwezesha kuwa na nguvu na afya bora wakati wa mwezi huu mtukufu
 
Usiruke Daku wakati wa Ramadhan



Kama kifungua kinywa chochote kilivyo na umuhimu katika sehemu ya mlo wa siku, Daku (chakula kinacholiwa kabla ya kupambazuka) ni mlo muhimu sana wakati wa mwezi huu. Husaidia sana mwili wako kubakia kuwa na maji, nguvu na virutubisho muhimu kwa siku nzima mpaka wakati wa futari. Pia chakula hiki kitakuepusha na kula kupita kiasi wakati wa kufungua swaumu yako jioni. Chakula kizuri cha daku kinaweza kujumuisha — Vyakula vyenye wanga, Vyakula vyenye asili ya nyuzi nyuzi mfano viazi, tende, viazi, mboga mboga n.k, na vyakula vyenye protini mfano mayai, jibini, nyama au samaki — vyote hivi ni kwa ajili ya kuupa mwili nguvu na maji wakati wa mchana
 
FB_IMG_1565713258563.jpeg
 
Punguza Sukari na Vyakula Vya Viwandani

Epuka sana vyakula vya viwandani, vinavyotengenezwa kwa haraka (fast food) ambavyo vinatengenezwa kwa mafuta mengi, sukari na wanga. Vyakula hivi vina virutubisho kidogo sana. Pia epuka vyakula vya kukaanda na vile vinavyoandaliwa kwa mafuta mengi. Ikiwa vyakula hivi haviepukiki, basi unaweza kujaribu kupunguza ujazo wa mafuta unayoyatumia.

3. Jumuisha Matunda na Mboga Kwenye Mlo



Matunda na mboga ni muhimu wakati wa kula, na ni mbadala mzuri wa vitu vitamu vitamu vinavyoliwa wakati wa mwezi wa Ramadhan. Baadhi ya matunda na mboga yana maji mengi, mfano matango, machungwa namatikiti maji, na. Ukila matunda haya wakati au baada ya kufuturu yanaweza kukufanya uwe na maji ya kutosha mwilini hadi kesho yake wakati wa futari.
 
Kula Futari Polepole na Usizidishe Chakula

Japo inashawishi kula mpaka uchoke wakati wa kufturu kutokana na kushinda njaa siku nzima, kumbuka kuwa unatakiwa uanze pole pole. Unaweza ukaanza na tende au maji kidogo kabla ya kula mlo kamili. Tende zinasifika kwa uwezo wake wa kuleta nguvu mwilini na pia kuandaa mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kwa mlo unaofuata. Baada ya hapo, unaweza ukafuata na kitu cha moto — mfano uji, maziwa, chai au supu. Kumbuka unatakiwa ule polepole ili kuupa mwili muda wa kumeng’enya chakula.
 
Zingatia Maji na Epuka Vinywaji Vyenye Kafeni



Japo unaweza ukahisi tumbo kujaa sana katika kipindi cha kati ya mlo wa ftari na Daku, usipuuzie kunywa maji maana yana umuhimu wake. Kunywa angalau glasi 4-8 za maji kwa siku. Tumia vimiminika au vyakula vyenye maji maji kwa kipindi cha kati ya futari na daku. Kuwa makini na epuka vyakula vyenye sukari nyingi na kafeni — vina vichocheo vinavyopelekea uhitaji mwingi wa maji mwilini. Ni vyema kuacha au kutumia kidogo tu vinywaji kama chai, kahawa, soda n.k
 
Moja ya vitu vizuri kuhusiana na sikukuu nyingi, ni jinsi zinavyotengeneza kumbukumbu na furaha zinazobaki kwa muda mrefu katika maisha. Na moja ya sikukuu ambazo zinabeba tamaduni za kipekee ni Pasaka. Ni sikukuu inayofuata baada ya mfungo wa waumini wa dini ya Kikristu na ni siku ya mapumziko kwa watu wa dini zote.
 
Andaa Chakula cha Pamoja



Katika kujumuika na uwapendao msimu wa sikukuu hii, andaa chakula cha pamoja kinachopendwa zaidi na watu wote. Pilau? Labda, lakini unaweza kufanya kitu cha tofauti msimu huu. Nyama choma na ndizi ama viazi, ama na mchanganyiko wa chakula kingine unaweza kuwa kiburudisho kizuri kwa ajili ya Pasaka hii. Wakati wakubwa wakiandaliwa nyama choma na vinywaji, unaweza kuwaandalia watoto chakula laini zaidi kama ndizi rosti na pilau kidogo. Kwetu uswahilini sherehe hainogi bila pilau.
 
Andaa Mchezo Utakao Waleta Karibu

Siku kama hizi za shehere ni vizuri kuweka majukumu mengine mazito pembeni na ku-enjoi pamoja na uwapendao. . Yapo mengi yanayoweza kuwleta watu karibu, michezo, filamu ama mazungumzo yaa furaha/ucheshi. Michezo kama mtu kati, kuchagua mtu na kumuuliza maswali magumu ni mchezo mzuri unaochangamsha. Kuangalia filamu nzuri za vichekesho ama muvi ya mateso ya Yesu Kristu kama ukumbusho wa sababu ya siku ya Pasaka kunaweza kuwa kitu cha kufanya na uwapendao. Katika kuchagua muvi ni vizuri kuzingatia muvi yenye maadili na mafunzo inayoweza kuangaliwa na watu wa rika lote.
 
Toa Zawadi na Pongezi



Fanya Pasaka hii ya kukumbwa na kila mtu kwa kutoa pongezi na zawadi. Hakikisha umeandaa kitu cha kukumbukwa na wana familia yako. Zawadi inaweza kuwa kitu chochote kitachobeba kumbukumbu kwa mpokeaji na mtoaji. Unaweza kuandaa vifaa vya shule kwa watoto na kuwapatia siku ya Pasaka kama zawadi. Mama anaweza kupewa doti ya vitenge, na baba anaweza kuzawadiwa saa ya mkononi. Kwa zawadi za mavazi tembelea zoomtanzania na fanya chaguo lako kua rahisi kutoka kwenye bidhaa nyingi zilizopo.
 
Sio zawadi za vitu tu. Hata maneno mazuri ya pongezi na shukrani kwa uwapendao yanaweza kuwa zawadi tosha. Andaa neno la shukran kutoka moyoni.i. Pia unaweza kuandaa neno ama tafakari nzuri itayoweza kumgusa kila mtu na kufanya siku hii kuwa ya pekee na chachu ya mabadiliko katika maisha yake.
 
Back
Top Bottom