Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Moja ya siku muhimu sana katika kalenda ya Kiislamu ni Eid al-Fitr. Husherekewa siku mbili, kuhitimisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao hudumu kwa mwezi mmoja. Tuangalie kwa umakini tamaduni za sikukuu hii, ambazo kwa asili yake husherekewa na familia, na jamii.
 
Eid al-Fitr Inaashiria Mwisho wa Ramadhan



Eid al-Fitr hufanyika siku ya kwanza ya Shawwal, mwezi wa Kiislamu unaokuja moja kwa moja baada ya Ramadan. Wakati wa Ramadhani, Waislamu wanalazimika kuacha kula, kunywa na shughuli nyingine za dhambi. Ni lazima kuzingatia hili ili kupata wakati wa kutafakari na kuabudu. Ukijulikana kama Mwezi Mtakatifu wa Kiislam, Ramadhan inaashiria wakati ambapo Quran takatifu ilifunuliwa kwa nabii Muhammad (saw).
 
Haiwezi Kuanza Mpaka Mwezi mpya Umeonekana

Kalenda ya Kiislam huongozwa na kuzama na kuchomoza kwa mwezi. Hii ndio sababu Eid al-Fitr huanguka siku na tarehe tofauti katika kalenda ya kawaida (Gregory) kila mwaka. Kwa mujibu wa tamaduni, Eid al-Fitr haiwezi kusherehekewa mpaka mwezi mpya umeonekana kwa macho ya kawaida (bila kutumia darubini). Hivyo ni kawaida kabisa kwamba sehemu fulani za ulimwengu zinaweza kusherehekea Eid al-Fitr tarehe tofauti na wengine. Mwaka huu, Eid al-Fitr inatazamiwa kusherekewa kati ya tarehe 4, 5 au 6 ya mwezi Juni.
 
Tafsiri Yake Ni ya Sikukuu Ya Kuvunja Saumu



Baada ya kujikataza kula chakula na maji wakati wa masaa ya mchana kwa mwezi mzima, Waislamu wengi wanafikia wakati wa kuvunja ibada yao ya kufunga. Inatafsirika kama “Sikukuu ya kuvunja Saumu,” vyakula vina nafasi muhimu sana siku hii ya Eid al-Fitr. Kifungua kinywa cha asubuhi kina umuhimu wake, ikijumuisha vitu vitamu vyenye sukari. Kwa Tanzania, utasikia vitu kama ‘Maadazi ya Eid’ kalimati na chai ya Maziwa. Kisha, familia zinakusanyika kwa chakula cha mchana siku hiyo hiyo baada ya sala ya asubuhi. Vyakula vya kila aina vya kikabila huliwa katika sherehe hii ya ya kufurahisha, huku watu wa dini mbalimbali wakijumuika na familia za Kiislamu kusherekea siku hii.
 
Nguo Mpya na Zawadi ni Utamaduni wa Eid al-Fitr

Pia siku ya Eid al-Fitr ni desturi ya watu kuvaa mavazi ya aina mpya. Katika dini ya Kiislamu, hupewa tafsiri kama sehemu ya kumuheshimu Mwenyezi Mungu na inalenga kuashiria wazo la upya wa nafsi kwa Muislamu aliyesamehewa dhambi zake mwezi wa Ramadhan. Pia, siku hii hujumuisha zawadi hutolewa kwa watu waote. Kama ilivyo kwa sikukuu ya Krismasi katika ulimwengu wa Kikristo, siku ya Eid al-Fitr ni wakati ambapo Waislamu wanaweza kuwaonyesha upendo wapendwa wao kwa zawadi. Watoto hupata zawadi zaidi, ingawa zawadi hutolewa kati ya marafiki na ndugu na watu wasio na uwezo.
 
Kutoa Hakuangalii Uwezo wa Familia



Waislamu wote wenye uwezo wa kifedha wanapaswa kulipa Zakat al-Fitr, aina ya sadaka maalum ambayo inalenga kuimarisha uhusiano ndani ya jamii ya Kiislamu na hisia za undugu na upendo. Mfumo huu huwawezesha watu masikini kuingizwa katika sherehe za Eid al-Fitr, kwa nia ya kuhimiza watu wenye uwezo wa kifedha kuwa na ukarimu zaidi mwaka mzima.
 
Ni Sherehe ya Watu Wote na Sio Waislamu Tu

Eid al-Fitr inaadhimishwa kama sherehe ya umma ili kujenga maana zaidi kwa jamii. Maonesho mazuri huendelea kipindi hiki, viwanja vya michezo ya watoto, mashindao tofauti n.k hufanyika katika maeneo ya umma.. Salamu kuu ya siku hiyo huwa ni “Eid mubarak” (Sikukuu Njema). Sikukuu huendelea vizuri hadi usiku. Pia katika sehemu nyingi za dunia, watu wa dini tofauti wanahimizwa kutembelea nyumba za marafiki zao wa Kiislam na kujiunga katika sherehe kwa kufurahia mlo wa siku hiyo na kubadilishana zawadi.
 
Kupata muda wa kufurahi na familia yako wakati wa Ramadhan inaweza kuwa changamoto. Ukifikiria muda kazi, muda wa kufuturu, muda wa ibada za usiku kucha, unaweza kudhani kuwa hauna muda kabisa kwa ajili ya familia. Lakini, mwezi huu ndio mwezi ambao ni muhimu sana kupata muda nao., Ni muda ambao unaunganisha familia na Mungu wao.
 
Katika kufurahia mwezi huo na familia, unaweza kuamua kuwatoa nje kwa ajili ya kubadilisha mazingira na kula mlo wa ftari tofauti na waliouzoea. Pia ni wasaa mzuri wa kuwapumzisha wanaoandaa ftari kila siku. Ikiwa ungependa hili, basi ni muhimu kuzingatia mambo yafuatayo:
 
Chagua Eneo/Mgahawa Wenye Mandhari Rafiki Kwa Kifamilia



Wakati wa kuchagua sehemu ya kwenda kupata ftari na familia, ni muhimu kuzingatia uwezo wa mgahawa kuhudumia familia familia nzima. Zingatia vitu kama umbali wa eneo, kelele, huduma, usafi, wapishi n.k. Pia baadhi ya sehemu zinaweza kuwa na meza zenye uwezo wa kuwahudumia watu wachache tu kwa wakati mmoja, hivyo ni muhimu kujua kabla ya kufika ili kuepusha usumbufu.. Unaweza kushirikisha familia yako wakati wa kuamua eneo la kwenda ili kila mtu afurahi.
 
Fanya Hifadhi (Booking) ya Meza ya Familia Mapema

Baada tu ya kuamua sehemu mnayotaka kwenda, piga simu kwenye mgahawa huo na kufanya hifadhi (booking) kwa ajili ya familia. Unaweza kupata namba za simu za mgahawa unaoutaka kwenye orodha ya namba za migahawa katika mtandao wa ZoomTanzania. Wasiliana nao kuwajulisha idadi ya wanafamilia mtakaokuwepo, na pia kuwajulisha kama kuna aina ya mkao mtakaochagua kuandaliwa. Mfano, kuna baadhi ya migahawa ina meza ndogo na haiwezi kuhudumia meza ya watu 10 kwa wakati mmoja. Lakini kuna baadhi ya migahawa inaweza kuunganisha meza au kuwekwa meza zinazokaribiana. Ukiwasiliana na wahudumu mapema na mkaelewana basi ni rahisi kufanya hifadhi.
 
Jua Orodha na Bei za Vyakula Vinavyoandaliwa



Tofauti na baadhi ya migahawa ambayo huwa inauza aina fulani ya vyakula tu, mfano Pizza, Kuku n.k, baadhi ya Migahawa na Hoteli huwa na mlo maalum mwezi huu wa Ramadhani. Wengi huwa na menu za kujichagulia (Buffet) kwa ajili ya ftari. Menyu ya buffet hiyo kwa kawaida huwa na vianzio mfano uji, chai, maziwa — kisha milo kama biriani, viazi, mihogo, kababu, kuku wa kuungwa n.k. Unaweza kuwapigia kuulizia menyu ya mwezi huu wa Ramadhan au kuangalia katika orodha mbali mbali katika mtandao.
 
Hakikisha Mnafika Kwa Wakati

Kwa kawaida kukutanisha wanafamilia, ndugu na jamaa sio kitu rahisi. Katika kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhan, kila mwanafamilia anaweza akawa anatokea upande wake, au kunaweza kuwa na mpango wa kukutana nyumbani na kuondoka kwa pamoja. Kama ni hivi, ni vema kufika eneo la tukio kwa wakati na kwa pamoja. Fikiria, kama mmeweka oda ya chakula cha watu 8, kisha watu 6 wakawahi kufika wakati wa kufuturu, kuna usumbufu mkubwa wa kusubiri. Ni muhimu kama unapanga kuitoa familia yako kuhakikisha watu wote wanafika kwa wakati. Pia kama mnatoka pamoja, basi ni vema kuzingatia bugdha kama foleni, kwa miji mikubwa mfano Dar es Salaam.
 
Kuwa Na Uvumilivu



Msimu huu wa Ramadhani, migahawa na sehemu nyingi za chakula zinakuwa na watu wengi sana hasa wakati wa kufuturu. Hii inapelekea wakati mwingine vyakula kupungua au kuchelewa kidogo kutokana na wingi na ukubwa wa oda. Ni muhimu sana kuzingatia hili hasa unapotoka na familia yako kula ftari. Kubali kuwa mwelewa ikitokea umeagiza kichwaji au chakula na kikachelewa kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…