Hakikisha Vioo Havina Ukungu na ni Visafi
Mwonekano mzuri ni muhimu sana wakati wa kuendesha gari, hasa msimu wa mvua. Ni muhimu sana kuhakikisha vioo vya gari lako havina aina yeyote ya uchafu, tope, unyevu au ukungu wakati unaendesha. Kama kioo cha gari lako kina hitilafu yeyote inayokuzuia kuona vizuri, basi rekebisha mapema kabla msimu wa mvua haujaanza. Na katika matumizi ya vifuta maji (windowscreen wipers) za kioo cha mbele na nyumba, hakikisha zinasafisha vyema ama ubadilishe mapema. Vifaa vingi vya magari vinapatikana mitandaoni, unaweza kuagiza au kuita fundi wakufungie.