Idadi ya vifo vya ajali ya lori la mafuta ya petroli lililoanguka kisha kuwaka moto eneo Msamvu mkoani Morogoro imeongezeka na kufikia 93 baada ya majeruhi wengine wanne kufariki leo Ijumaa Agosti 16,2019.
Vifo hivyo vinafanya idadi ya wagonjwa waliobaki kuwa 21 kati ya 46 waliokuwa wamefikishwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu.
Akizungumza baada ya kutembelea wagonjwa hao leo Ijumaa Agosti 16, 2019, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema madaktari wanafanya kila jitihada kuokoa maisha ya wagonjwa waliobaki.