Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mtag
IMG_20190816_165433.jpeg
 
Angalia Betri na Mfumo wa Umeme Mapema

Kwa kawaida, betri za gari zimetengenezwa kudumu kati ya miaka minne mpaka sita . mvua inaweza kuathiri ubora wa betru yako. Maji maji na unyevu vinaweza kusababisha kutu na shoti katika sehemu tofauti za gari lako (mfano kama kuna nyaya zilizochubuka) na hivyo kuua betri ndani ya muda mchache. Katika kuelekea msimu wa mvua, ni bora kulifanyika kazi hili mapema. Kama gari linaonyehsa dalili yeyote ya kusumbua katika mfumo wa umeme au betri kusumbua wakati wa uwashaji gari ni bora kuingia gharama mapema. Ni afadhali kutumia pesa sasa hivi kuliko kulala barabarani ndani ya gari lililozimika usiku wakati wa mvua.
 
Kagua Mfumo wa ‘Suspension’



Huwezi kusahau kabisa mfumo wa ‘Suspension’ wakati wa msimu wa mvua. Maji husifika kwa uharibifu wake hasa katika sehemu za vyuma. Katika mfumo wa uendeshaji, sehemu kubwa ya ‘Suspension’ imefunikwa kwa mipira na plastiki ili kuzuia maji yasiingie. Lakini wakati mwingi, mipira hii huzidiwa na joto na hivyo kupasuka. Hivyo, hakikisha mapema sana, kabla msimu wa mvua haujafika unapeleka gari lako kukaguliwa hasa sehemu hizi zinazohitaji kufunikwa na mipira bado ziko imara. Vinginevyo, gharama za kurekebisha zinakuwa kubwa zaidi wakati wa kubadilisha vifaa vya chuma badala ya mipira midogo midogo.
 
Kufanya mauzo mtandaoni kunajumuisha mafunzo mengi ambayo unaweza kujifunza endapo tu utafanya biashara. Idadi ya wafanyabiashara mtandaoni inaongezeka kila siku. Baadhi wanafanikiwa sana na wengi wanaishia njiani.
 
Kagua Mfumo wa ‘Suspension’



Huwezi kusahau kabisa mfumo wa ‘Suspension’ wakati wa msimu wa mvua. Maji husifika kwa uharibifu wake hasa katika sehemu za vyuma. Katika mfumo wa uendeshaji, sehemu kubwa ya ‘Suspension’ imefunikwa kwa mipira na plastiki ili kuzuia maji yasiingie. Lakini wakati mwingi, mipira hii huzidiwa na joto na hivyo kupasuka. Hivyo, hakikisha mapema sana, kabla msimu wa mvua haujafika unapeleka gari lako kukaguliwa hasa sehemu hizi zinazohitaji kufunikwa na mipira bado ziko imara. Vinginevyo, gharama za kurekebisha zinakuwa kubwa zaidi wakati wa kubadilisha vifaa vya chuma badala ya mipira midogo midogo.
 
Miongoni mwa sababu ni kushindwa kujifunza kwa wafanyabiashara juu ya nini kinafanya kazi, na nini hakifanyi. Kama ukiepuka makosa haya, unaweza kuingia katika kundi la wafanyabiashara wa mtandaoni waliofanikiwa zaidi

Haya ni makosa 5 ambayo wengi wanayafanya wakati wakijaribu kuuza vitu mtandaoni
 
Kutegemea Kupata Wateja Kwa Haraka



Kufanya mauzo mtandaoni ni zaidi ya kupiga picha na kuziweka mtandaoni tu. Watu wengi wanaamini kwamba, ukiwa na bidhaa ukaiweka mtandaoni basi wateja watamiminika. Inaweza kuonekanai ni kazi rahisi sana. Lakini kwa uhalisia inahitaji “sadaka” kubwa zaidi.

Badala yake, unatakiwa kuzingatia kutengeneza na kukuza jamii ya wanunuzi wako kwanza. Waoneshe thamani ya kuwa katika kurasa za mitandao yako ya kijamii. Unaweza kufanya hivi kwa kuwaonesha a video au kuwaandikia makala zinazowaelimisha na zenye thamani kwao. Mfano, kama unafanya biashara ya nguo, unaweza kuandaa video au kuandika makala kuhusiana na mitindo iliyoko kwenye chati, njia mbalimbali za kuwaa mrembo n.k. Kwa kufanya hivi, unatengeneza jamii inayokuamini na itakuwa rahisi kwao kununua bidhaa kutoka kwako.
 
Kuwauzia Watu Ambao Hawapo

Kama hujui watu unaowauzia/kuwatangazia bidhaa yako, ni kama unawauzia wateja ambao hawapo. Na kujaribu kuwauzia wateja ambao hawapo, si tu unapoteza muda, bali ni kigezo kikubwa cha kutofanikiwa.

Kama unauza bidhaa maalum, anza kwa kujifunza wateja wako walipo. Mitandao ya kijamii imegawanyika. Watumiaji wa mitandao hiyo wamegawanyika vile vile. Ni kama soko la Kariakoo, kuna upande utakua unauza nguo sana, kuna upande unauza vitu vya elektroniki, na kuna upande unauza vifaa vya ofisini tu. Peruzi Twitter, Instagram, magrupu ya Facebook ili kujua.Kama unauza magari, kuna magrupu Facebook ya wauzaji na wanunuzi wa magari. Jiunge na magrupu ili kujifunza jinsi watu wanavyouliza maswali katika mitandao tofauti, vitu wanavyopenda n.k. Hii itakuwezesha kujua jinsi unavyoweza kuingiza biashara yako katika maisha yao ya kila siku.
 
Kutoelewa Msaada Unaohitaji ili Kuendesha Biashara Yako



Biashara ya mtandaoni ni kubwa. Na kama unaamua kuingia kuifanya, basi ni vema kujua ni msaada . Kama unaamua kufungua tovuti na mitandao ya kijamii kwa ajili ya biashara yako, tafuta mtaalamu wa kukusaidia. Kama unaona hautaweza kuendesha mitandao ya kijamii peke yako, tafuta mtu wa kukusaidia. Ni vigumu kufanya kila kitu kuanzia kuhudumia wateja (wanaopiga simu na wanaotuma meseji kwenye mitandao ya kijamii), kufanya mauzo na matangazo n.k
 
Kama umeamua kuwekeza katika biashara ya mtandaoni, basi ni vyema pia kutenga bajeti kwa ajili ya rasilimali watu. Unaweza kuandaa fungu kwa ajili ya watu watakaokusaidia katika kuunda na kuendesha mitandao yako. Kufanya hivi kunaweza kukusaidia kushughulikia mambo yale ambayo yanaweza kukuza biashara yako
 
Kushindwa Kutoa Kipaumbele kwa Huduma kwa Wateja

Kosa kubwa linalofanywa wakati wa kuanzisha biashara ya mtandaoni ni kuweka bidhaa bila kujali huduma kwa wateja.. Kwa mazingira ya Kitanzania ambapo bado wateja wengi wana wasiwasi na masoko ya mtandaoni kwa ukionyesha dalili yeyote ya kushindwa kumridhisha basi unaweza kumkosa.
 
Kama unauza vitu mtandaoni, ni muhimu kujua nje ndani juu ya bidhaa yako. Unaweza ukawauzia watu kitu au huduma na maswali yakawa mengi juu ya matumizi. Kama utashindwa kujibu utaonekana mbabaishaji. Jifunze kila kitu kuhusu bidhaa yako, maswali wanayoweza kukuuliza, changamoto n.k. Itakuwa rahisi sana wakipiga simu kuuliza maswali utaweza kuwasaidia. Hii itawatengenezea moyo wa kukuamini na kukutegemea. Mara nyingine wakitaka kitu/huduma, lazima wagonge mlango wako
 
Back
Top Bottom