Baada ya kutajwa mara kwa mara kuwa kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane yupo katika matatizo na rais wa klabu hiyo, Florentino Perez, Zidane amekana hawana matatizo yoyote.
Inatajwa sababu kubwa iliyoibuka wawili hawa kuwa katika matatizo ni baada ya Zidane kumuhitaji kiungo wa Manchester United, Paul Pogba lakini Perez alishindwa kukamilisha usajili huo.
"Nimekuwa katika wakati mzuri na rais wetu, yeye ndio aliyenileta mimi hapa kucheza jambo hilo siwezi kulisahau hata kidogo, kila mtu yupo huru hapa kwa siku zote," alisema.
Akizungumzia maneno yanayosemwa na watu wanaomzunguka kwamba yupo katika matatizo na rais huyo, alisema hakuna jambo hilo na wala hayapi nafasi maneno hayo.
"Siangalii watu wanasema nini nje ya hapa, naweza nikachukulia poa na wala halinusumbui, kitu ambacho kinasumbua ni kazi yetu ya kila siku na hii nafasi ambayo nimeipata kuwa kocha wa hapa," alisema Zidane.
.KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola amemtetea staa Alexis Sanchez akisema kwamba kuboronga kwa mchezaji huyo huko Manchester United halikuwa kosa lake.
Sanchez ameondokana na balaa la Man United baada ya kukamilisha uhamisho wake wa mkopo wa msimu wote wa kujiunga na Inter Milan katika dirisha hili la majira ya kiangazi.
Wakati fowadi huyo wa kimataifa wa Chile akilalamikiwa kila kona kwa kukosolewa kwamba kiwango chake kibovu kufuatia kucheza hovyo tangu alipotua Old Trafford akitokea Arsenal Januari, 2018, Guardiola ameibuka na kusema wanaopaswa kulaumiwa ni Man United.
Ni mtu safi, mtaratibu na mpambanaji. Na sasa ameamua kwenda Italia kujiunga na moja ya timu kubwa Ulaya kwa sasa, Inter Milan, akicheza chini ya kocha mkubwa Antonio Conte.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.