Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

 
Wewe hujiachii kama wale. Mada zao za mara kwa mara na zenye mlengo mmoja. Comments zao zile zile...Manengelo hasa hasa kwenye ujasiriamali na Demiss kwenye zile ishu zake...Wewe siyo rahisi kuku-categorize....
Manengelo na kwenye ule Uzi wa pombe
Ila demiss anaweza kuwepo anapita tu kimya kimya bila matashtiti😂 ila nimemmiss na nyuzi zake
 
Maoni ni sehemu muhimu ya ukuaji wa kazi zako kitaaluma. Huonyesha ikiwa utendaji wako ni mzuri au mbaya na ni maeneo gani unapaswa kuboresha. Kupokea maoni hasi kazini inaweza kuwa ni kitu kigumu kusikia, lakini ni fursa ya kujifunza na kutumia somo utakalolipata kuwa mfanyakazi mzuri zaidi.
 
Jipe Muda Na Nafasi ya Kutosha Kutafakari



Wakati wa ukiwa unapewa maoni juu ya kazi yako, unaweza kuwa na hisia sana. Inawezekana ukashindwa kuendelea kumsikiliza bosi wako au ukachagua kujibishana nae. Hii inaweza kukufanya ukose maelezo ya muhimu au kusababisha kutokuelewana. Ni muhimu kujipa wakati na nafasi ya kutosha ili kuchuja na kupokea vyema maoni hayo. Hii itakusaidia kupata muda mzuri kufikiria juu ya hali hiyo kwa uwazi zaidi na kupanga majibu yanayojiridhisha. Unaweza kuomba muda wa kukusanya mawazo yako kabla ya kujibu maoni hayo..
 
Tambua Vitu Chanya tu Kutoka kwenye Maoni

Maoni ni kitu muhimu kwa ukuaji wako binafsi na wa kitaaluma. Hata wakiyawasilisha kwa njia nzuri au mbaya, meneja au mfanyakazi mwenzako watakupa maoni mabaya ili uweze kufanya kazi bora zaidi. Ili kusimama imara juu ya taaluma yako, chagua kutenga na kuchukua maoni chanya na ufanyie kazi bora zaidi.
 
Fikiria ni Kwa Nia njema



Njia nyingine ya kubakia kuwa mchapakazi hata baada ya maoni hasi ni kwa kufikiria juu ya nia njema ya bosi au mfanyakazi mwenzako kwanza. Maoni ni ishara kwamba wanataka kukusaidia kufanya kazi bora ambayo itasababisha kufanikiwa katika kazi yako. Ikiwa utaona kuwa watoa maoni wana nia nzuri na wanaweza kukusaidia kuleta matokeo bora, itakuwa rahisi kwako kufanya mabadiliko mazuri.
 
Sikiliza kwa Makini

Kubishana na mfanyakazi au meneja wako kwa sababu ya maoni yao, hata kama ni hasi haitasaidia. Wanaweza kuwa na mawazo ambayo yangekusaidia kufanya kazi bora, lakini wakashindwa kufanya hivyo. Badala ya kujitetea sana au kupambana na kubishia maoni yao, jaribu kuwasisitiza kwa upole wakupe maelezo zaidi. Uliza maswali kama ‘Unaweza Kunipa ufafanuzi zaidi? Una sampuli ya kazi kama hiyo? Unaweza kunionyesha mfano ili nifanye vizuri zaidi?’ Kwa njia hii, utakuwa na uwezo wa kuifanya kazi hiyo vizuri zaidi.
 
Back
Top Bottom