Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Boateng, 32, alisema akiwa amecheza mechi 14 tu kwenye timu alitaka kuonyesha umahiri wake afahamike kwamba yeye ni mfalme kwa kuamua kununua magari matatu siku moja, akisema: “Nilikuwa mjinga na kuishi kama mfalme.”
 
Staa huyo alisema hiyo na sababu nyingi kadhaa ndizo zilizomfanya ashindwe kuishi kwa furaha Spurs na hivyo kupata wakati mgumu ndani ya uwanja
 
Ninachoweza kusema kwa sasa ni kwamba sikulichukulia soka kama kazi. Nilikuwa mjinga sana, nilikuwa na kipaji, lakini sikufanya mazoezi kwa sana, nilitaka kuwa uwanjani kwa saa moja tu,” alisema.
 
Nilikuwa nafika wa mwisho mazoezi na wa kwanza kuondoka. Nilikuwa kwenye mitoko tu na marafiki. Nilikuwa na pesa, naishi kama mfalme. Sikuwa nakwenda gym. Jambo hilo lilibadili kabisa maisha yangu ya soka ya baadaye.
 
Boateng amepita kwenye klabu 12 tofauti, lakini furaha ya maisha yake ya soka alikuja kuifaidi kidogo akiwa tayari umri umeshakwenda, wakati alipokipiga Las Palmas na Sassuolo kisha kutua kwa mkopo Barcelona kabla ya sasa kujiunga na Fiorentina.
 
Back
Top Bottom