Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Griezmann bado anatafuta namna ya kutuliza maisha yake huko Barcelona baada ya kujiunga na timu hiyo akitokea Atletico Madrid kwa ada ya Pauni 107 milioni. Staa huyo Mfaransa ametua Nou Camp baada ya sakata la muda mrefu la uhamisho wake huku staa Messi alichokuwa akitaka ni klabu hiyo kumrudisha Neymar kikosini.
 
Griezmann alisema: "Messi sio mtu anayependa kuzungumza sana na mimi nipo hivyo, hivyo inakuwa ngumu. Niliwahi kumpa chai, nadhani mwelekeo wetu ni mzuri. Lakini, amekuwa akipata sana majeruhi, hivyo tunashindwa kuwa na muunganiko ndani ya uwanja ili kufanya urafiki kushamiri.

"Sisi ni watu wawili safi kabisa, na ukweli nipo hama kusaidiana na yeyote kwenye timu."
 
Messi hakutumika sana kwenye mechi za mwanzoni mwa msimu kutokana na kuwa majeruhi, huku Griezmann, ambaye amefunga mabao matatu katika mechi nane alizocheza Barca anamtaka Muargentina huyo arudi haraka uwanjani ili watengeneze kombinesheni itakayowafanya kuwa marafiki na kuzungumza mara kwa mara.
 
Back
Top Bottom