Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuna watu ambao wao ni wakuzaji wa mambo.

Hawa ni wanyonya nguvu pia ambao wao kitu au jambo dogo hufanywa kubwa hadi mtu anaweza kuamini kwamba ni jambo kubwa kweli, ingawa awali alijua ni jambo dogo. Hawa wako maofisini na majumbani. Mtu anaumwa na mafua, lakini atalalamika, atagumia na kuaga kabisa na kuacha kabisa wosia, kwamba anakufa.
 
Yeye mwenyewe huyu anayefanya visa hivyo anaamini kwamba, kwa kufanya hivyo, atapata huruma zaidi, ataona watu wanavyohangaika kuonesha wanavyomjali na kutaka kupima umuhimu wake. Kwa kawaida kukuza kwao mambo kunaweza hata kusababisha hata wengine wakaugua zaidi au hata kupoteza maisha kabisa, kutokana na kuongeza chumvi sana kwenye maneno yao.
 
Kuna wale ambao kwa lugha ya mtaani tunawaita wameza kaseti.

Hawa ni wale ambao wanataka waongee wao tu, wanataka wao ndiyo wasikilizwe na mwingine anapotaka hata kusema moja hapewi nafasi. Mtu atazungumza yeye kuanzia mwanzo hadi mwisho, hata kama ni kwa saa tatu mfululizo. Mwingine anapotaka kuongea, yeye ameshamkatisha na kuzungumza yeye. Hataki kuona mtu mwigine akizungumza kama yeye yupo. Hata kama ni mgeni mahali, akishapewa nafasi ya kuzungumza, huzungumza kweli.
 
Hajali kama kuna mtu ambaye anataka aseme hisia zake, hapana. Inafika mahali, kama unamsikiliza unachoka kabisa. Hatajali, hata kama utamwonesha kutokujali. Kama ni nyumbani au ofisini, hatajali kukupotezea muda wako kwa vyovyote vile. Kama ni ushauri aliomba kwako, yeye ndiye atakupa ushauri kwa sababu, hatakupa nafasi ya kuzungumza katika kumshauri. Hawa ni wanyonya nguvu ambao tunao kila siku.
 
Kuna wanyonya nguvu ambao kazi yao ni kuwafanya wengine washitakiwe na dhamira.

Kila wakati linapotoea jambo , juhudi yao kubwa ipo kwenye kutafuta njia ya kulaumu ili wengine washitakiwe na dhamira. Wakati mwingine jambo liko wazi kabisa kwamba, hao anaowalaumu hawahusiki, lakini ni lazima atalaumu tu. Hata kama atafafanuliwa na kuona kwamba, anaowalaumu hawana tatizo, bado atasema, ‘hata kama hamtaki anahusika kidogo’Wanyonya nguvu hawa wanatafuta kasoro ili walaumu, ili mtu mwingine ajisikie kukosa, ashitakiwe na dhamira.
 
Inasikitisha sana bro. Kahama, Geita na Kule Mara kukoje. Wanawalazimisha angalau kutoa huduma muhimu za kijamii karibu na hiyo migodi au mambo ni yale yale? Mambo haya ndiyo alikuwa anapigania Ken Saro Wiwa dhidi ya kampuni la Sheli huko Nigeria mpaka wenye mafuta yao wakamuua.

Williamson alimpenda sana huyo demu wa kifalme na alisikitika alipoambiwa kuwa asingeweza kumuoa kwa sababu yeye, pamoja na mialmasi yake yote, hakuwa na damu ya kifalme. Siyo kamji tu ila Ulaya na Marekani zote zimejengwa kwa utajiri wa Afrika na mataifa mengine masikini. Na hali hiyo inaendelea. Ndiyo maana akitokea kiongozi wa Kiafrika mzalendo akaanza kuhoji hii mifumo ya kinyonyaji wanamwondoa fasta sana !!!
Mambo ni yale yale bro,, huduma nyingi za kijamii hali ni mbaya na kwa wiki lazima ndege zichukue mizingo ya kutosha tu..

Bado kuna shule hazina madawati, suala la afya tete, barabara mbovu na kubwa zaidi ni kuachiwa mashimo ya kutosha
IMG20190104072100.jpeg
 
Anaweza kuangalia mtu anavyofanya kazi Fulani na kuona ni nzuri sana. Lakini atajaribu kwa kadiri awezavyo kumkosoa mtu huyo kwa kitu ambacho wala wakati mwingine hakihusiani moja kwa moja na kazi ile. Anaweza kusema ‘ile kazi ya mwaka jana angefanya hivi tusingekosa tenda’ lengo ni kumfanya mtu ashitakiwe na dhamira. Hataki kusifia hii kazi nzuri ya sasa, anataka kukosoa ya zamani ambayo iliharibika.Dawa ya hawa ni kuwapuuzia.
 
Back
Top Bottom