Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Utafukuzwa kazi. Mkuu keshapongeza. Nawe pongeza tu yaishe. Bla bla zako za sijui sheria hairuhusu zitakuponza [emoji16][emoji16]
IMG-20191004-WA0020.jpeg
 
Mkataba wa straika huyo utafika tamati mwishoni mwa msimu 2023-24, lakini mpango wa mshambuliaji huyo kwa sasa ni kushinda mataji, hivyo huenda akachukua jambo hilo na kutafuta timu itakayompa nafasi hiyo ya kutamba kwenye mataji.
 
BADO yupo. Ndiyo, bado yupo sana. Kama wewe ulikuwa ni shabiki wa Manchester United unayeombea Kocha Ole Gunnar Solskjaer afukuzwe, basi utasubiri sana. Habari za ndani kutoka klabuni hapo zinadai mabosi wa United hawana mpango wa kumfuta kazi.
 
United imeanza vibaya msimu huu huku katika ligi ikiwa imekusanya pointi tisa katika mechi saba za mwanzo. Na kumekuwa na uvumi huenda klabu hiyo ikafanya uamuzi mgumu wa kumfuta kazi Solskjaer ambaye ni staa wake wa zamani klabuni hapo.
 
Makocha, Thomas Tuchel wa PSG na Massimiliano Allegri ambaye hana timu baada ya kuachana na Juventus wamekuwa wakihusishwa na kibarua hicho cha Old Trafford endapo Solskjaer ataendelea kufanya vibaya lakini habari za ndani kutoka United zinadai mabosi wa timu hiyo bado wana imani naye.
 
Maisha yamekuwa magumu kwa makocha waliokuja baada ya kumalizika kwa zama za kocha maarufu wa zamani, Sir Alex Ferguson ambaye aliondoka mwaka 2013 akiiacha klabu hiyo ikiwa bingwa wa Ligi Kuu. Lakini mpaka sasa hakuna kocha aliyefanikiwa kufuata nyayo zake.
 
United imefukuza makocha watatu tangu kuondoka kwa Sir Alex Ferguson ambapo kocha wa kwanza kupoteza kazi yake mapema alikuwa mrithi wake, David Moyes aliyedumu klabuni hapo kwa miezi 10 tu ingawa alikuwa na mkataba wa miaka sita.
 
Kocha mkongwe wa Kidachi, Louis van Gaal alidumu kwa muda mrefu zaidi baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa misimu miwili lakini alifukuzwa Mei 2016 baada ya klabu hiyo kumaliza katika nafasi ya tano na kushindwa kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa.
 
Mourinho alianza vema maisha yake ya soka Old Trafford huku akichukua Kombe la Ligi pamoja na Kombe la Europa ambalo liliipa nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa wa Ulaya msimu uliofuata. Hata hivyo, Desemba 2018 alifukuzwa klabuni hapo baada ya timu kujikuta katika mwenendo mbovu huku kocha huyo akiwa haelewani na mastaa wake.
 
Na sasa mzigo mkubwa kwa sasa umeamwangukia Solskjaer ambaye ameendelea kuandamwa na matokeo mabovu licha ya kuanza vema pindi alipochukua nafasi ya Mourinho Desemba mwaka jana. Baadaye mambo yalianza kwenda kombo kuelekea mwishoni mwa msimu ambapo United ilishindwa kupata nafasi nne za juu.
 
Back
Top Bottom