Mohamed Salah –(Chelsea)
Kwa sasa supastaa, Mohamed Salah anatamba akiwa na kikosi cha Liverpool, ambako amekuwa akiwatambia tu Chelsea kwenye mechi wanazokutana kwenye Ligi Kuu England na michuano mingine. Lakini, kabla ya hapo, Mo Salah alikuwa kwenye kikosi cha Chelsea alikoonekana hafai na kupigwa bei kwa ada ya Pauni 16 milioni kwenda AS Roma. Kipindi hicho, Chelsea ilikuwa chini ya Jose Mourinho na hiyo ilitokea baada ya kumtoa kwa mkopo Mo Salah timu kadhaa ikiwamo Fiorentina na AS Roma kabla ya kuuzwa jumla. Ubora mkubwa huko kwenye Serie A uliwafanya Liverpool kufungua pochi na kwenda kunasa saini yake, ambapo sasa amewafanya wakali hao wa Anfield kutamba tu.