Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Thorgan hazard
Huyu ni mdogo wake, supastaa Eden Hazard na walitua Chelsea kwa wakati mmoja mwaka 2012. Lakini, Thorgan hakupata kabisa fursa ya kuitumikia Chelsea, ambapo hakucheza mechi yoyote hadi hapo alipouzwa kwenda Borussia Monchengladbach kwa ada ya Pauni 5.9 milioni. Baada ya kutua huko kwenye Bundesliga, hakika Thorgan amekwenda kuwa bonge la mchezaji na kuzifanya timu kibao kuhitaji huduma yake na hivyo kubadili tu timu, huku ubora wake wa kiuchezaji ukifananishwa na ule wa kaka yake ambaye pia ameachana na Chelsea na sasa anakipiga Real Madrid. Kina Hazard wana mdogo wao mwingine anaitwa Kylian Hazard ambaye pia ni moto
 
Juan Cuadrado – (Chelsea)

Staa wa Colombia, Juan Cuadrado alitua kwenye kikosi cha Chelsea akiwa na matumaini makubwa ya kufanya kweli baada ya kutamba kwenye fainali za Kombe la Dunia 2014 huko Brazil. Lakini, kilichotokea alijikuta akicheza Stamford Bridge kwa msimu mmoja tu, 2014-2015 kabla ya kupigwa bei kwa ada ya Pauni 17 milioni, akinaswa na Juventus, ambako wamekwenda kumfanya kuwa wing-back wa kushoto na hakika amewafanyia huduma bora kabisa. Staa huyo hadi sasa amekuwa mtu muhimu huko Turin, akisaidia timu hiyo kubeba mataji kibao kwenye Serie A, huku akiwatesa mabeki wa timu pinzani hadi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kutokana na kasi yake.
 
Iago Aspas – (Liverpool)

Mhispaniola huyo alisajiliwa na Liverpool kwenye majira ya kiangazi mwaka 2013 baada ya kufanya vizuri alipokuwa na kikosi cha Celta Vigo. Lakini, mambo hayakwenda vizuri kwa Aspas huko Anfield na matokeo yake kujikuta akitolewa tu kwenye timu hiyo, ambapo alicheza mara tano tu katika kikosi kilichoanza.
 
Mashabiki wa Liverpool lazima watakuwa na mshangao kuhusu Aspas kwa namna alivyokwenda kurudi kwenye ubora wake huko kwenye La Liga na kufunga mabao ya uhakika aliporejea zake Celta Vigo, kumfanya arudishwe kwenye timu ya taifa ya Hispania na kwenda kuwafunga bao England uwanjani kwao Wembley.
 
[emoji943]
tapatalk_1542556164546.jpeg
 
Suso – (Liverpool)

Suso alinaswa na Liverpool kipindi hicho akiwa na miaka 16, ambapo kocha Rafa Benitez alimshawishi kusaini huko Anfield, akienda kuungana na Mhispaniola mwenzake. Kufikia mwaka 2012, akaanza kutumika kwenye kikosi cha kwanza huko Anfield, lakini kwa wakati huo kocha alikuwa Brendan Rodgers.
 
Alicheza vizuri sana kwenye mechi yake ya kwanza alipowakabili Manchester United, lakini baadaye akaanza kupigwa benchi, kitu ambacho kimemfanya staa huyo kutolewa kwanza kwa mkopo Almeria. Baadaye, akatua Milan ambako anacheza soka lake matata kwelikweli na kutajwa kuwa mmoja wa wanasoka mahiri kwenye Serie A kwa sasa.
 
Jambo hilo lilimfanya kocha Wenger amfungulie mlango wa kutokea Mjerumani huyo katika msimu wa 2014/15. Kwanza ilikuwa kwa mkopo huko West Brom ambako pia kocha Tony Pulis alimwona kuwa hafai kucheza kwenye Ligi Kuu England ndipo Arsenal walipoamua kumuuza jumla kwenda Werder Bremen ya Ujerumani ambako baada ya muda mfupi tu akawa mkali kinoma. Sasa, anakipiga huko Bayern Munich na shughuli yake pevu kiasi cha kuanza kufukuziwa na Real Madrid.
 
Mtoto halisi wa Finland

Jina lake halisi ni Teemu Eino Antero Pukki na alizaliwa Machi 29, 1990 katika mji wa Kotka nchini kwao Finland. Alianza kucheza soka lake la utotoni katika kituo cha HOPS kilichopo mjini kwao Kotka. Baadaye akajiunga katika klabu ya KTP na kucheza katika kikosi cha chini ya miaka 19.
 
Alicheza kikosi hicho akiwa na miaka 16 tu na kiwango chake kikasababisha acheze timu za vijana za taifa za Finland. Alipopandishwa timu ya wakubwa alicheza Ligi Kuu ya Finland kwa misimu miwili akifunga mabao matatu katika mechi 29.

Anaswa na Sevilla achemsha, arudi kwao
 
Hatimaye Pukki alinunuliwa na Sevilla ya Hispania akitokea KTP na alijumuishwa katika mechi ya kwanza katika pambano la ugenini dhidi ya Real Madrid Desemba 7, 2008. Aliishia benchi. Alicheza mechi ya kwanza Januari 25, 2009 katika pambano dhidi ya Racing. Baadaye aliishia kucheza timu ya akiba na mwisho alirudi kwao Finland.
 
Agosti 28, 2010 Pukki alisaini mkataba wa miaka mitatu na nusu na klabu ya HJK Helsinki ya Finland. Mwaka 2011 alifunga mabao 11 huku akipika mabao nane katika mechi 18 za Ligi. Alichaguliwa katika timu ya msimu ya Ligi ya Finland. Alikuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha HJK Helsinki ambacho kilishiriki michuano ya Ligi ya mabingwa na kisha Europa.
 
Alifunga mabao mawili dhidi ya bangor City katika ushindi wa mabao 2-0 lakini pia akafunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Schalke nyumbani. Akafunga bao pekee katika kichapo kikali cha mabao 6–1 walicholambwa ugenini na Schalke.
 
Schalke 04 yamnasa

Kutokana na mabao yake hayo matatu dhidi ya Schalke klabu hiyo ya Ujerumani iliamua kumnasa Agosti 31, 2011 akisaini mkataba wa miaka mitatu. Novemba 6, alifunga mabao mawili katika pambano lake la kwanza dhidi ya Hannover 96.
 
Back
Top Bottom