Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa kufunga mabao hayo mawili alikuwa mchezaji wa tatu wa Finland katika historia ya Bundesliga kufunga mabao mawili ndani ya mechi moja. Wengine waliowahi kufanya hivyo hapo awali ni Ari Hjelm na Pasi Rautiainen.
 
IMG_20191005_144326.jpg
 
Atinga Celtic

Agosti 31, 2013, Pukki alitua katika klabu ya Celtic ya Uskochi kwa dau ambalo halikutajwa. Alifunga bao katika pambano lake la kwanza tu dhidi ya Hearts mnamo Septemba, 14, 2013. Akafunga tena katika pambano lililofuatia dhidi ya St Johnstone Septemba 21. Januari 26, 2014 akafunga dhidi ya Hibernian.
 
Julai 8, 2014 akaifungia Celtic Hat trick katika pambano la maandalizi ya msimu dhidi ya LASK Linz ambapo walishinda 5–2. Akafunga mabao mawili katika pambano la kufuzu Ligi ya mabingwa wa Ulaya dhidi ya KR Reykjavik. Hata hivyo baadaye akajikuta amepoteza fomu yake klabuni hapo.
 
Atinga kwa mkopo Brøndby ya Denmark

Septemba Mosi 2014 baada ya kuchemsha na Celtic, Pukki alisaini mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja katika klabu ya Brøndby IF ya Denmark huku klabu hiyo ikipewa fursa ya kumchukua jumla mwishoni mwa msimu.
 
Alimaliza msimu akiwa mfungaji bora wa klabu akifunga mabao tisa. Juni 19, 2015, Pukki alisaini mkataba wa miaka mitatu kukipiga Brøndby. Julai 31, 2017 alifunga bao moja dhidi ya VPS katika pambano la kwanza la kufuzu michuano ya Europa 2017–18 huku Brøndby wakishinda 2–0. Mei 10, 2018 alicheza pambano la fainali kombe la Denmark wakishinda 3-1 dhidi ya Silkeborg IF.
 
Norwich yamnasa, atesa

Juni 30, 2018 Pukki alijiunga katika klabu ya daraja la kwanza ya Norwich City akiwa mchezaji huru huku akisaini mkataba wa miaka mitatu. Alicheza mechi ya kwanza Agosti 4 katika sare ya 2-2 dhidi ya Birmingham City. Wiki moja baadae akafunga bao lake la kwanza katika kichapo cha mabao 4-3 nyumbani dhidi ya West Bromwich Albion.
 
Back
Top Bottom