Juan Cuadrado – (Chelsea)
Staa wa Colombia, Juan Cuadrado alitua kwenye kikosi cha Chelsea akiwa na matumaini makubwa ya kufanya kweli baada ya kutamba kwenye fainali za Kombe la Dunia 2014 huko Brazil. Lakini, kilichotokea alijikuta akicheza Stamford Bridge kwa msimu mmoja tu, 2014-2015 kabla ya kupigwa bei kwa ada ya Pauni 17 milioni, akinaswa na Juventus, ambako wamekwenda kumfanya kuwa wing-back wa kushoto na hakika amewafanyia huduma bora kabisa. Staa huyo hadi sasa amekuwa mtu muhimu huko Turin, akisaidia timu hiyo kubeba mataji kibao kwenye Serie A, huku akiwatesa mabeki wa timu pinzani hadi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kutokana na kasi yake.