Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

DAVET mbona hivi?
1570373241748.png
 
ameandika farrel JNR

Imenikumbusha hadithi ya Galileo Galilei, yeye alikuja na tafsiri mpya juu ya suala la jua na dunia kuhusu kipi kinamzunguka mwenziwe.
Ushahidi wake mkubwa aliujenga katika utafiti wa maji kupwa na kujaa; hili lilitokana na dunia kulizunguka juwa huku ikijizungusha yenyewe na ndio sababu ya mabadiliko baina ya usiku na mchana na msimu wa hali ya hewa tafauti.
 
Aliposimama tena akiwa na ushahidi mkubwa zaidi wakamshitaki na kukutikana na hatia ya uzushi dhidi ya dini na wakamfunga kifungo cha ndani mpaka alipofariki dunia. Nadharia yake haikuishia jelani, waliomuamini wakaja na hii “E pur si muove” wakimaanisha dunia bado inazunguka kila juwa linapochomoza.
 
Hadithi hii inafanana na yanayomkuta Dr Mwele, aliekuwa mkuu wa taasisi ya masuala ya tafiti za maradhi ya kuambukiza. Alifukuzwa kazi baada ya kusema kuwa ugonjwa wa Zika uliingia nchini na juzi kabatizwa jina kama la Galileo kuwa ni mzushi tena basi msaliti anaetumiwa na mabeberu.
 
Shutuma za juzi zinaonyesha wateuzi hawakupendelea yule mama kuendelea kujipatia rizki ya halali baada ya kuchaguliwa na dunia kuongoza sekta hio Umoja wa Mataifa. Twab’an alitakiwa awe miongoni mwa wale wa kupiga magoti na kubusu pete kidoleni mwa mtukufu.
 
Unaweza kuwa na mtazamo tafauti juu ya msimamo wa Dr Mwele kutangaza uwepo wa Zika nchini. Na zaidi suala la teuzi analo mteuzi na ni hiyari yake. Ila kumnanga hadharani mmoja wa wanasayansi wanaoheshimika duniani kwa chuki za ajabu ili tu kumshusha heshima na kumuweka katika hali ya hatari kwa wavamizi waliotangaziwa hadharani kuwa ni msaliti anaetumiwa na mabeberu ni jambo lisokubalika na ovu.
 
Msingi mmoja wa ubobezi wa taaluma (Intellectualism) ni hoja na ushahidi (reason and rational) si nguvu na kejeli kwa kila unalolipinga. Inasikitisha zaidi na kutia khofu ikiwa nadharia za aina hii zinabebwa na “wabobezi wa taaluma” dhidi ya wengine tena wote wakiwa ni wanasayansi. Inakufanya ufikiri tunapoelekea na nafasi ya taaluma pamoja na wanataaluma dhidi ya wanasiasa na nguvu walizonazo.
 
Back
Top Bottom