Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

#Fursa

Kwa ufupi Brexit inaweza kurejesha fursa bora zaidi kwa wananchama wa Jumuia ya Madola. Maana huko nyuma kulikuwa na mpaka bango maalum mpakani linalosema njia hii ni kwa Muingereza na wale wote wanaotoka katika jumuia ya Madola (UK and Commonwealth) na lengine likisema kwa kwa waliobaki. Kwa sasa linasema Umoja wa Ulaya (UK & EU) na waliobaki. Mfumo wa uhamiaji baada ya hii “free movement” imeuathiri zaidi wageni wa kiafrika ambao visa zao za shule zilifutwa, hata wagonjwa wa miaka na dahri nao ghafla wakaanza kukataliwa ruhusa ya kuingia kwa sababu kubwa ya sehemu unayotokea.
 
#MiakaMiwili

Hapa chini kuna mabadiliko ya kisera inayosema mwanafunzi mgeni ataruhusiwa kuishi miaka miwili baada ya kumaliza masomi yake. Ahadi hii imekuja kwa sababu ya Brexit maana wanajuwa “free movement” inaondoka na kutakuwa na hitajio la wageni, wale ambao wanaweza kuwaambia kaeni au ondokeni badala ya wale ambao wanabaki kuwa wahamiaji wa kudumu kwa sababu ya makubaliano ya uanachama walionao kwenye EU.
 
Jnr Farrell
September 4 ·
#Afrikakulikoni

Ya Afrika Kusini na haya ya Brexit yanafanana kwa moja ambalo ni suala la wageni na kazi. Kelele za wenyeji ni wingi wa wageni na anguko la kazi kwa mnasaba wa kuwa wageni wameshika kazi wakati wenyeji hawana. Ukitazama kwenye Brexit utaona suala la wahamiaji kutoka nchi wanachama (free movement) ndio msingi wa maamuzi ya kujitoa katika umoja wao. Japokuwa wako wanauzungumzia kuporwa kwa mamlaka yao na Brussels lakini kiini cha yote ni hasa ongezeko la wageni kutoka nchi hasa za Ulaya ya Mashariki.
 
#Mtazamo

Lakini tazama sasa jinsi gani sehemu hizi mbili zinakabiliana na suala la uhamiaji. Afrika Kusini wao wameamua kuuwa kwa ukatili wa hali ya juu watu wanaofanana nao kwa kila kitu, kuanzia rangi, silka, utamaduni na yote yanayowatambulisha kama Waafrika. Wameacha magenge ya vijana kuuwa, kubaka, kuiba na kila ovu kama vile ambavyo apartheid ilivyowafanyia wazawa na dunia ikasimama nao dhidi ya uonevu na ukatili waliokuwa wakifanyiwa.
 
#Brexit

Kwa huku waingereza wao kwanza wametafuta jina la kuhamasisha azma yao, BREXIT. Wakafanya kura ya maoni ya kujitoa, na sasa wamo katika msuguano wa wenyewe kwa kwenyewe namna ya kijiondoa katika kiini wanachokiona kuwa sababu ya mashaka ya uhamiaji na ongezeko kubwa la watu linalowasumbua. Si aghlabu ukayaona yanayotokea Afrika Kusini hivi leo yakatokea katika nchi zao. Hutasikia mroma, mpolish na wengine wakaachwa wapigwe, wauawe, wabakwe, wavunjiwe majumba na kuibiwa mali zao kwa sababu ya uhamiaji.
 
mwaka jana mulibahatika walipoteza point ovyo sasa sijui mwaka huu kama watarejea tena kosa.
naomba ukalale kabla moudgulf hajatoka kwenye shimo lake.

jamaa ana makero kama mlevi wa kipemba
Ata msimu huu watapoteza tena hawana pumzi ya kukimbia mbio ndefu hao
IMG-20190922-WA0011.jpg
 
#Akhlaq

Hizi ndio tafauti za akhlaki baina ya sisi waafrika na hawa wanaoitwa mabeberu. Utu hatuna hasa miongoni mwa waafrika kwa waafrika, hatuna hisani, hatuna heshima ya maisha baina yetu wenyewe waafrika wala hatuna wema wa moyoni baina yetu wenyewe. Kile kile walichokuwa wakifanyiwa katika apartheid nao wanakifanya kwa wengine. Si aghlabu muafrika akamuonea beberu, mara nyingi ni muafrika dhidi ya muafrika, lazima mmoja abebe utukufu wa kumuonea aliedhaifu miongoni mwa waafrika wenzake.
 
#Afrika

Tatizo la Afrika nzima ni namna tulivyoupa mgongo utu na ubinaadam. Hatujawa na ustaarabu wa kusimamisha haki kwa nidham na kwa makusudi tunakuwa wepesi wa kuchaguwa nguvu. Mfano mdogo majuzi unasikia Mkuu wa Wilaya akisema wezi waachwe wapigwe na wauawe kwa sababu mahakama huwaachia huru. Tena anatangaza kabisa hata akiiba senti moja, ameamua kuiba na hivyo ameamua kuua au kuuawa. Haya mambo yanapozoeleka ndio huzaa maovu mengine. Unapowaaminisha watu kuwa sheria haziko kwa maslahi yao basi kilichobaki ni sheria mkononi mwa watu. Hivi haya ya Afrika Kusini yanatafauti gani na wanyama mbugani na “dominance” ya dume moja katika himaya yake?
 
#Mabeberu

Tunaowaita mabeberu na udhaifu wote walionao bado wanaheshimu sheria zao ambazo misingi yake ni huru katika haki na utu. Kwenye Brexit wameamua kubadili sheria wakabiliane na mashaka ya uhamiaji kisheria badala ya kuacha makundi maovu kuingia mitaani na kuuwa watu wao wenyewe. Sisi Afrika hatuwathamin raia wetu wenyewe itakuwa mgeni? Mfano wa haya ya Afrika kusini ni kauli tata za baadhi ya viongozi. Unaposema mitumbwi ya wageni izamishwe kwa vile ni wavamizi haramu unatafauti gani na hawa wa Kusini wanaochoma wahamiaji moto na kuwafukuza na visu mitaani? Unapookota maiti za “wahamiaji” waliowekwa kwenye viroba wakiwa wamefungwa kamba miguuni na wala huumizi kichwa kujuwa sababu za miili ile kuwapo fukweni unategemea nini?
 
#Haki

Bila ya misingi imara ya haki hatuwezi kuwa na tafauti na wanyama. Unapokuta jambazi anachomwa moto hadharani na jamii ikichekea basi juwa ule msemo wa “Jungle Law and the survival of the fittest” umeshabeba utamaduni tena wa kurithishana. Na ndio mwisho wake jamii katili huzaliwa ikiwa tayari kuchinja hata vichanga, walemavu na wazee kusaka utajiri wa kishirikina. Na maendeleo makubwa ilio nayo Afrika Kusini, siamini abadan kama haya yaliofanyika yasingeweza kuzuilika ila maslahi ya kisiasa na ukosefu wa utu umelitia dosari taifa kubwa barani Afrika na ikiwa hali itaachwa iendelee basi nayo itajikuta ikiwa sawa na wengine barani Afrika wanaorudi nyuma badala ya kusonga mbele.
 
Tatizo kubwa ni khulka yake ya ubabe, uonevu, ukatili na ukosefu wa utu. Khulka hii imekuwa kubwa ikibeba upevu wa ufisadi si wa mali pekee bali ni ufisadi mbaya zaidi wa utu. Ukweli ni kuwa “The thrill is gone”, hakuna tena zile hashtags, hakuna alie salama hata miongoni mwao wenyewe. Wito kwa sasa ni Katiba mpya itayosimama kwenye misingi ya haki na uhuru wa haki.
 
Barakat l’eid

L’aeidina minalfaizyna”. Maneno ya wenyewe wa rahatu zaman, wakati huo tushatazama mwezi kuandama pale forodhani na mizinga hupigwa kuashiria siku kuu ya Eid el fitr.

Mtaani ni harufu tu ya vanila, katika mahanjumati tafauti. Mtaa mzima ni vileja, keki, mkate wa kusukuma, sambusa, katlesi na kila lililo na utamu usiomithilika. Kwetu kaskazini lazima ukutane na mashikio, aina ya vileja hivi vikubwa vilivyowekewa sukari ya unga juu.
 
Siku hizi maneno yamebadilika, Eid Mubarak imejaa mitandaoni na ndio wataalam wanapoita “evolution” ya lugha. Wale wa barakat l’eid wamepunguwa maana kipindi chao cha makubadhi ya ngozi ya ng’ombe na buibui la kamba kimepita kama upepo na gharika zake
 
Sawa pia na maamkizi ya “Subalkheyr na msaalkheyr yenye asili ya swabahal kheyr na masa al’kheyr maana ya asubuhi na jioni njema. Wapo wachache wanaoitumia misamiati hii, mara ya mwisho nimeisikia Malindi na pia kwa mmoja wa marafiki zangu anapozungumza na mzee wake.
 
Kuna maamkizi kama cheichei, shikamoo na marahaba. Haya yanakupa uhalisia wa makaazi ya msemaji, cheichei ni kwa mji mkongwe na jamii zake za mjini. Shikamoo ni kwa mitaa ya kati, ng’ambu na mashamba. Na wa mjini usimpe shikamoo, washamba usimjaribu kwa cheichei, mnaweza msifahamiane.
 
Salam alaykum imekuja miaka ya 80 mwisho na kutiliwa mkazo zaidi na walimu wa madrasa katika kipindi cha changamoto za taaluma pana za kiimani hasa katika ufaham wa masuala ya mwezi, bidaa na makuzi ya wahitimu wapya wa taaluma za thiolojia ya kiislam, wale waliokuja na shahada na stashada za Misr, Sudan, Madina na Kuwait.
 
Mfano marehem Ustadh Majid, miongoni mwa wahitimu wa mwanzo wakiwa na “Masters” za thiolojia ya imani yetu. Almarhum sheikh Abdulrazak nae akawa mudir pale Chuo cha Kiislam, Marehem Pandu wa Pandu akawa Naib wake. Nakiita kipindi cha sheikh Nassor Bachu, mmoja wa wahadhir alieitikisa Zanzibar ya miaka 80 na mchango wake mkubwa wa kukuza hoja na changamoto zilizokuja baina ya mazowea, imani na dini.
 
Miaka hio simu zilikuwa za TTCL za ndani, mkono wake mweusi na jumba lake ni ima jekundu au kijani. Baadhi ya sehemu zilijengewa vibubu hivi na kufuli ili usiweze kupiga bali upokee tu, gharama wakati huo za simu hazikushikika. Ikapigwa simu nyumbani siku ya Eid, mpigaji akasema Eid Mobarak, ndugu yangu akamjibu Edi Mbaraka hakai hapa, anakaa kule! Sababu ni kuwa neno hili bado lilikuwa geni, tulizowea zaidi kusikia Barakat l’eid. Edi Mbarak alikuwa ni jirani yetu pale Mazizini. Kipindi cha Air Tanzania, Virgin Butterfly na sheikh Abdulwakil Nombe.
 
Back
Top Bottom