Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Sawa sawa na hadithi moja ya mzee wa kimanga na mtoto wa kishingwi. Alipofika katika nyumba akapiga hodi, akamuuliza yule mtoto wa kishingwi, Baba yako yupo? Akamjibu “Kawamoo”, yeye akasikia kama Shkamooo. Akamjibu Marhabaaa, baba yako yupo, ikawa ndio ya kuku na yai “Kawamooo”. La haja zetu, unaweza kumkuta wa Nungwi wewe mjini usimfaham, huko kusini ndio hakusemeki. “Jaje, kulamku” au wale wa “wabesa na Bwaganchakase”, halkadhalika na kwa wale “wakati wa vita chonga mbele, sasa wewe mpupi hupai”. Yaani mzee wa kimakonde wakati wa vita Kagera ilikuwa anaambiwa asonge mbele, sasa hatakiwi jeshini kwa vile mfupi.
 
Kwa sisi wa mji mkongwe tuliosoma katika madrasa za msikiti Meman pale Mkunazini, Eid Mobarak haikuwa ngeni. Nakumbuka mpaka leo ile “Tum konho, Musalman”. Tulikuwa na maalim wetu akitufunza urdu kwa maandishi na mikwaju, ujue kukisoma na kukizungumza. Jamii za kizanzibari zilibeba baadhi ya matamshi ya asili zao, mfano wangazija wengi hasa sehemu za msikiti nambar huku mpaka leo ukiwakuta watu wazima utawasikia “Kwezi”, “Ngaliwa mnono”. Wazungu wanasema “Diversity” kwa maana ya mchanganyiko wa jamii tafauti na raha za kinachoitwa “cosmopolitanism”.
 
Naam, hata miaka yetu ya thamanini tuliwahi raha za jirani goa na umaridadi wa mavazi ya Jumapili, wauza mikate wa kimanga, madobi wa kibaniani, wabarawa na maduka yao ya soda na “Imports”, washihiri na migudulia ya kahawa, wazaramo na sherehe zao, wa mashamba na dhikr zao halkdhalika wauza mafuta ya nazi na mkoba wa ukili na wale wa maziwa ya ng’ombe na mitungi yao juu ya kibao cha nyuma cha “Raleigh”.
 
Zanzibar ni njema, na wema wake upo katika ustaarabu unaoanza na lugha, mavazi, akhlaq na nyendo. Ukitazama mapenzi ya Zanzibar kama nchi hayakuja tu kama mvua bali yamejengewa misingi ya uwepo wake katika zama tafauti na jinsi aila tafauti na ile “Bottle neck effect” ilivyoacha alama mpya ya Zanzibar kama watwan ya wazanzibari.
 
Jnr Farrell
April 13 ·

#Poyoyo
Ni mtu aliekula chumvi ya kutosha lakini akabaki na mawazo mgando yasioendana na uhalisia wa maisha aliyopitia kwa kadri ya umri wake. Tafauti yake na nyumbu ni kuwa nyumbu hufuata upepo unapoelekea akisaidiwa sana na udogo wa maarifa na hasa pale anapokosa nyenzo za kufikiri mbali.
 
Tuunge mkono juhudi...[emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji23]
Screenshot_20191006-181026_Twitter.jpeg
 
Sleeping with the fishes: Africa's first underwater hotel
The first underwater hotel in Africa has opened off the remote island of Pemba, part of the archipelago of Zanzibar, in Tanzania.
The hotel is 250m (820 ft) out to sea and consists of three floors, including a dining room and an upper deck for star-gazing. The bedroom is below deck completely submerged by water and provides a 360-degree view of sea life.

✔✔
 
#Jamii

Jamii inayopata tabu zaidi ni ile ilio na nyufa hasa za wenye mamlaka ya maamuzi iliosheheni poyoyo. Maana katika fikra za poyoyo ni kuwa zama zake yeye alikwenda shule miguu peku, akarudi hana chakula, na leo hii ni balozi wa nyumba kumi. Iweje wewe udadisi haki ya ubora wa maisha kuliko poyoyo aliehangaika na akafika?
 
Ndio ukakuta mathalan unaweza kuwa na mtaa wa Mwenyekiti poyoyo wenye kisima cha maji na mashine ya kusukuma maji kijiji kizima lakini poyoyo akaizima isitumike kabisa kwa sababu itachakaa na kuharibika.

Hutabasam rohoni kila nyumbu anaepita na doo lake kichwani akiimba na kusifu hekima za poyoyo muona mengi. Mantik ya poyoyo ni ubwana wa zamu, lakini jamii iliobaki iteseke.
 
#Afrika

Maendeleo duni barani Afrika ni kwa sababu ya poyoyo waliosoma kwa wakoloni wakalalamika mateso yaliowakuta lakini wakayatenda yale yale ya mateso kwa vizazi vilivyotarajia mema baada ya kuondoka ukoloni. Ndio utakuta poyoyo haondoki madarakani mpaka afikwe na tahayur ya kuondoshwa kwa nguvu za wale wale waliokuwa wakimlinda akiwapika katika uzalendo wa nyumbu ngamani.
 
#Muflis

Upoyoyo ndio uliolipelekea bara la Afrika likawa masikini kwa wananchi wake lakini tajiri kwa neema lilizojaaliwa zikawafaidisha wengine. Upoyoyo ndio uliokuza utumwa, naam kwani hujui machifu wetu wenyewe walitajirika kukamata na kuuza wasiowapenda miongoni mwa wananchi wao? Upoyoyo ndio ulioleta ukoloni na leo hii ukoloni mamboleo unakuzwa zaidi na upoyoyo wa “system” zetu.
 
Back
Top Bottom