Kwa wenzetu huko. Utamaduni mzuri. Ukiboronga kidogo tu unaachia madaraka. Ricky Perry, waziri wa nishati wa Trump kajiuzulu. Kosa lake? Kumshauri vibaya bosi wake kuhusu skendo ya Ukraine inayotishia hata kumwondoa madarakani.
Kwa nini inakuwa hivi? Mimi naamini kuwa, pamoja na ukomavu wao wa demokrasia, wanasiasa wao wengi mara nyingi siyo hohehahe. Hawategemei vyeo vyao ili kuendesha maisha yao. Wengi wao wana pesa zao tayari na wanakubali vyeo hivi kama priviledge tu ili kuimarisha profiles zao, na kukuza majina ya familia; na kujenga destiny. Ni tofauti sana na sisi huku ambako siasa na uongozi ndiyo mtaji wa mtu anaoutegemea kumtajirisha. Akijiuzulu atakwenda kutajirikia wapi?
Mpaka leo huwa namshangaa Nyerere kwa kusisitiza kuwa ili kuwa kiongozi ilikuwa lazima uwe masikini; na wakati huo huo anakutegemea uwe mwadilifu kweli kweli usiibe. Ndiyo maana hakuwa na mfuasi wa kweli hata mmoja katika itikadi zake hizi za ajabu....
View attachment 1236934