Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

MWENYE pesa unaambiwa sio mwenzako. Hilo ndilo linalofanya klabu za soka duniani kutofautiana. Kuna zile zinazotengeneza vikosi vyao kuwa moto mkali kutokana na kuwa na pesa nyingi na kuna nyingine ambazo zimekuwa zikiungaunga na kuwa na timu zenye makali ya kawaida tu.
 
Kutokana na hilo, ligi nyingi za huko Ulaya zimeshuhudiwa mastaa kibao wakisajiliwa kwa pesa ndefu na hiki hapa ndicho kikosi kilichonaswa kwa pesa nyingi zaidi kwenye historia ya Ligi Kuu Ufaransa (Ligue 1), akiwamo Msenegali, Idrissa Gueye.
 
Kipa aliyebeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2017/18, Keylor Navas aliachana na Real Madrid na kutua Paris Saint-Germain mwaka jana baada ya kuitumikia timu hiyo kwa miaka mitano. Kipa huyo aliondoka Bernabeu baada ya kupigwa benchi na kipa Thibaut Courtois na PSG walimnasa kwa Pauni 14 na kumfanya kuwa kipa ghali kwenye historia ya Ligue 1.
 
David Luiz

beki wa kati

(Chelsea kwenda PSG)

Ada: Pauni 40 milioni

Paris Saint-Germain ililipa pesa nyingi kumsajili David Luiz kutoka Chelsea mwaka 2014 na hakika alikwenda kuwasaidia kubeba mataji kadhaa kwenye kikosi hicho hasa katika ligi. Kwa kipindi hicho, ada hiyo iliweka rekodi ya dunia huko Ufaransa hasa kwa mchezaji anayecheza kwenye nafasi ya beki na hivyo kumfanya Mbrazili huyo kuingia kwenye orodha hii matata.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
FB_IMG_1571415865176.jpeg
 
Thiago Silva

beki wa kati

(AC Milan kwenda PSG)

Ada: Pauni 33 milioni

Moja ya mabeki bora kabisa kwenye kizazi chache. Thiago Silva ni beki kisiki kwa klabu yake na timu ya taifa, ambapo hakika anapokosekana uwanjani basi pengo lake limekuwa dhahiri kabisa. Kwa muda mrefu amekuwa akitambulika kama beki bora na hilo liliwafanya PSG kumsajili kwa pesa nyingi, Pauni 33 milioni ilimponasa kutoka AC Milan na hivyo kumfanya kuwa mmoja wa wachezaji ghali huko Ufaransa.
 
Thilo Kehrer

Beki wa kati

(Schalke kwenda PSG)

Ada: Pauni 33 milioni

Alinaswa na Paris Saint-Germain kwa ajili ya matumizi ya baadaye. Thilo Kehrer ni kiraka ambaye anaweza kucheza kwenye nafasi nyingi kwenye beki, kuanzia kati na pembeni. Msimu uliopita hakupata nafasi sana ya kucheza, lakini kiwango chake bora kimemfanya kucheza mechi saba kwenye timu ya taifa ya Ujerumani, huku huduma yake ikinaswa kwa pesa nyingi zikimfanya kuwa mmoja wa walio ghali Ufaransa.
 
Back
Top Bottom