Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa wenzetu huko. Utamaduni mzuri. Ukiboronga kidogo tu unaachia madaraka. Ricky Perry, waziri wa nishati wa Trump kajiuzulu. Kosa lake? Kumshauri vibaya bosi wake kuhusu skendo ya Ukraine inayotishia hata kumwondoa madarakani.

Kwa nini inakuwa hivi? Mimi naamini kuwa, pamoja na ukomavu wao wa demokrasia, wanasiasa wao wengi mara nyingi siyo hohehahe. Hawategemei vyeo vyao ili kuendesha maisha yao. Wengi wao wana pesa zao tayari na wanakubali vyeo hivi kama priviledge tu ili kuimarisha profiles zao, na kukuza majina ya familia; na kujenga destiny. Ni tofauti sana na sisi huku ambako siasa na uongozi ndiyo mtaji wa mtu anaoutegemea kumtajirisha. Akijiuzulu atakwenda kutajirikia wapi?

Mpaka leo huwa namshangaa Nyerere kwa kusisitiza kuwa ili kuwa kiongozi ilikuwa lazima uwe masikini; na wakati huo huo anakutegemea uwe mwadilifu kweli kweli usiibe. Ndiyo maana hakuwa na mfuasi wa kweli hata mmoja katika itikadi zake hizi za ajabu....


View attachment 1236934
Wenzetu walishaendelea kitambo bro,,viongoz wangap baran Afrika wanafanya madudu lakini bado wapo madarakan?

Wamejaa kashfa za kila aina, lakin kung'atuka kwenye nafasi walizopo hawawez kujarbu hata kidogo,,njaa mbaya sana Bro,

Wapo kwa masirahi yao binafsi na sio kwa kulipigania taifa, pia bado hatujakomaa kwenye demokrasia
 
Ni mtazamo wako, me naiona kwa mtizamo huo wangu.
tapatalk_1443008349194.jpeg
 
Back
Top Bottom