Lakini Mungu ni nani hasa? Mungu ni Roho (Yohana 4:24) anayeishi katika ukamilifu wa milele, akiwa peke yake katika mbingu ya kwake mwenyewe, huku malaika na viumbe wengine wote wakiwa chini yake.
Kabla ya uumbaji Yehova alikuwa peke yake mbinguni akiishi katika ukamilifu wa milele. Lakini hilo halikumpendeza hata akaamua kuwa na msaidizi kwa ajili ya kazi maalumu ya uumbaji wa malaika na wa ulimwengu mzima. Mzaliwa wa kwanza wa Yehova (Wakolosai 1:15) anaitwa Yesu Kristo; ambaye Mungu alimuumba kwa mfano wako, ili asaidiane naye kumuumba binadamu kwa mfano wao.
Mamilioni ya watu wamechepuka katika mahusiano yao. Wengine wameua na imebaki kuwa siri yao. Wengi wanakwepa kodi ya serikali na hawakamatwi. Lakini hatuwezi kumdanganya Mungu. Kwa sababu anatujua hadi ndani ya mioyo yetu.
Mioyo yetu wenyewe hutudanganya kidogokidogo katika kutenda dhambi, wakati mwingine bila sisi wenyewe kujua. Lakini, iamini Biblia, Mungu hawezi kuichukulia dhambi kirahisirahisi! Kwa sababu anaupenda sana uumbaji wake.
Kuna kitu kibaya sana ndani ya mtu. Hilo liko wazi. Biblia inasema chanzo cha matatizo ya mtu ni moyo wake, roho yake, pamoja na uwezo wake wa kufikiri. Tumejaa ulaghai, unafiki na utata. Tunajichezea sisi wenyewe ule mchezo wa kitoto wa kombolela. Yaani, tunajificha na kujitafuta wenyewe, tunawadanganya watu lakini Mungu anatuona.
Labda ni katika mazingira hayo ambapo moyo hufanya kazi yake kwa uharibifu zaidi. Huficha uovu mkubwa wa dhambi unaoendelea kuwa mkubwa, na matokeo yake kuwa mabaya na mazito zaidi. Moyo unatulaghai katika kufikiri kuwa si mbaya, au kwamba Mungu ni mwenye huruma sana kiasi kwamba atapuuza.
Tusipoacha kutenda dhambi, dhambi haitakomeshwa. Ni wajibu wa kila mmoja wetu kukomesha dhambi katika maisha yake. Usisubiri wengine waikomeshe kabla au kwa niaba yako. Hata serikali haitaweza kukusaidia