Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Morogoro, SP Albert Kitundu (49) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe alikataa kuandika maelezo polisi na kudai atayatoa Mahakamani, kuhusu watu anaodai waliuliwa na Jeshi la Polisi kwenye operesheni Mkoani Kigoma.
_
Pia amedai katika upelelezi walioufanya wakati huo akiwa Msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi Kinondoni, alibaini kuwa kilichosemwa na Zitto hakikuwa na ukweli kwani watu waliofariki si 100 kama alivyodai bali ni wanne ikiwemo Askari Polisi wawili.
_
Hayo yamebainishwa na SP Kitundu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati akitoa ushahidi ambapo aliongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga.
_
Baada ya kutoa ushahidi huo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 22, mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa.
#MillardAyoMAHAKAMANI