Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Boresha maisha ya watu kwa kadiri utakavyoweza. Ukisaidia mtu 1 watahurumiwa watu 10. Ukisaidia watu 10 watahurumiwa watu 100. Ukisaidia watu 100 watahurumiwa watu 1000. Kila mmoja wetu akitambua wajibu wake katika jamii, Mungu atatuhurumia sisi wote. Maisha ya mtu mmoja yakiboreka, mmoja huyo ataboresha na ya wengine wengi. Hivyo, endelea kuogelea lakini usisahau kurudi nyuma katika jamii.
 
Muhogo ni zao la mizizi, ikiwa sehemu ya mmea ulio na jina la kilatini Manihot esculenta. Watu wanaoishi karibu na mabonde ya Mto Amazon huko Amerika ya Kusini waliishi kwa kula muhogo kwa mamia ya miaka kabla ya mvumbuzi Christopher Columbus kusafiri huko.
 
Zao la muhogo ni maarufu sana duniani kote na hapa kwetu nchini Tanzania kwa sababu ni zao gumu linalovumilia ukame na kustawi vizuri bila ya uhitaji mkubwa wa mbolea ingawa hushambuliwa kwa urahisi na magonjwa yatokanayo na bakteria na virusi.
 
Muhogo hutumikaje?
Wakazi wa kanda ya Ziwa Victoria nchini Tanzania wanafahamika sana kwa kula ugali unaandaliwa kutokana na unga wa zao la muohogo. Ni mojawapo ya vyakula maarufu sana katika mikoa ya Mwanza, Kagera, Kigoma, na Mara.
 
Hii ni kwa sababu muhogo na unga wa muhogo ni chanzo kizuri na rahisi cha wanga. Chakula hiki kinaweza kutoa kalori zaidi kwa ekari ya mazao kuliko mazao mengine ya nafaka kama vile mahindi na mtama. Kwa hivyo muhogo ni zao lililo na faida nyingi sana katika ulimwengu wa leo unaoendelea hasa Afrika na Tanzania ambako idadi ya watu inazidi kukua.
 
ameyataka Depal
BREAKING NEWS;
hatimaye kwa mara ya kwanza sembe limepanda thamani hadi kufikia 5000 mjini zanzibar
  1. sembe tupu kwa kopo la maji ya mfereji pamoja na chumvi ya madonge kwa mama wajawazito = shilingi 350 na sahani unakosha.
  2. sembe na kachumbari = 500 na maji ya kisima bure
  3. sembe na bamia = 500 na sahani unakosha
  4. sembe na maharage = 1500 na maji ya mto rufiji bure.
  5. sembe, nyama choma, maharage, mboga na pilipili, maji ya kiwandani = 5000 pamoja na risiti ya malipo.
 
Watu huandaa na kula chakula cha muhogo kwa njia mbalimbali katika sehemu mbalimbali za dunia, kuoka na kuchemsha zikiwa njia mojawapo. Katika maeneo mengine na hasa maeneo ya Ziwa Victoria, watu huvundika muhogo kabla ya kuutumia katika mfumo wa unga ufahamikao kwa jina maarufi la udaga.
 
Ni muhimu sana kuula muhogo ukiisha menywa na kuchemshwa, hasa aina ya muhogo mchungu. Hii ni kwa sababu aina nyingi za mbegu za muhogo mchungu zina sumu ifahamikayo kwa jina la cyanide ambayo inaweza kukuletea madhara makubwa ya kiafya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…